Salha Mohamed
Mwalimu Julius Nyerere |
ASKARI mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ), Mwanahamisi Musa amelalamika kutotimiziwa ahadi ya kujengewa nyumba
aliyoahidiwa na Baba wa Taifa, marehemu Mwalimu Julius Nyerere.
Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
aliyekuwa ziarani Pugu Stesheni mkoani humo juzi, Mwanahamisi anayekadiriwa
kuwa na umri wa zaidi ya miaka 80 aliyestaafu Jeshi mwaka 1984, alisema alipewa
ahadi hiyo kwa kuwa mwanamke wa kwanza wa JWTZ kufanya kazi kwenye kitengo cha
Rada za kuongozea ndege nchini, hivyo kuandika historia.
Alidai kuwa kutokana na nafasi hiyo, Mwalimu
Nyerere wakati huo akiwa Rais, alimwahidi nyumba kama shukrani za kutambua
mchango wake.
”Niliahidiwa na Nyerere kujengewa nyumba
kwa sababu nilikuwa mwanamke wa kwanza kusimamia Rada, lakini nasikitika ahadi
ya mzee… nasikia uchungu…kwa nini Mungu alimchukua kabla hajanikamilishia ahadi
yangu!” Alilalamika Mwanahamisi.
Alifafanua kwamba ahadi ya Baba wa Taifa
ilieleza kiuwa nyumba hiyo angejengewa nyumbani kwao Tabora na tayari alikuwa na
eneo la ujenzi alilopewa na Idara ya Ardhi ambalo hata hivyo, liliporwa na kuuziwa
mtu mwingine ambaye pia ameliuza.
Akijibu hoja ya Mwanahamisi, Makonda
alisema Rais John Magufuli anathamini michango ya wazee waliotumikia Taifa hili
pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,
Jenerali Davis Mwamunyange kuwa ni msikivu.
“Ikibainika ni kweli uliahidiwa
kujengewa nyumba hiyo na kuwa wewe ulikuwa mtumishi wa JWTZ tena mwanamke wa
kwanza kufanya kazi katika kitengo muhimu cha Rada, mimi nitakutafutia kiwanja
Tabora na nitakujengea nyumba ya vyumba
vitatu Tabora,” alisema Makonda na mstaafu
huyo kumshukuru.
0 comments:
Post a Comment