Salha Mohamed
Paul Makonda |
MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepiga
marufuku baadhi ya idara katika halmashauri za jiji kupewa fedha mara kwa mara
huku wahusika wanaotoa fedha hizo wakitegemea kupata asilimia kadhaa.
Makonda ametoa onyo hilo wakati akizungumza na watumishi
wa Manispaa ya Ubungo kupitia ziara yake ya siku kumi mkoani humo yenye lengo
la kusikiliza na kutatua kero na changamoto za wananchi ili kuzitolea
ufafanuzi.
Alisema zipo idara katika halmashauri ambazo hupewa
fedha mara kwa mara sababu ya kuwa na uhakika wa ulaji.
"Kuna baadhi ya idara hudai fedha hizo zimepelekwa
kwenye mradi wa maji au ujenzi wa barabara kwa madai kwamba ni barabara muhimu
kumbe wahusika wanamkataba na wakandarasi ya kwamba akipata fedha za malipo
asilimia fulani atoe kwao," alisema.
Kutokana na hali hiyo Makonda alisema anataka watu
waadilifu na wanaowajibika na kueleza kuwa ni vyema kuwatambua wanaofanya kazi
na kumsaidia Rais pamoja na kuwatambua wavivu na mizigo wanaokula fedha za
mshahara bila kufanya kazi.
Makonda alisema: "Ifikie wakati watumishi hao katika
kujiletea matokeo mazuri wajiulize kwamba wamehudumia watu wangapi katika ofisi
zao na si wamenufaika vipi na ofisi hizo," alisema.
Aidha aliwataka watumishi wa wilaya hiyo mpya ya Ubungo
kufanya kazi kwa uadilifu ili wananchi watamani kwenda katika manispaa hiyo
kupata huduma.
0 comments:
Post a Comment