Mwandishi Wetu, Rukwa
Loy Mhando |
MAJINA ya
biashara na kampuni 495 yamesajiliwa katika kipindi cha siku 90 za kampeni ya mkoa kwa mkoa
inayofanywa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), ili kuhamasisha
wafanyabiashara.
Kaimu Meneja
Miliki Ubunifu wa Brela, Loy Mhando, alibainisha hayo jana kwamba kati ya idadi
iliyosajiliwa, 72 ni kampuni na 423 ni majina ya biashara na kampeni hiyo imepata
mafanikio.
“Tunaendelea
vizuri, mwamko wa wafanyabiashara ni mkubwa kwani wanajitokeza,” alisema Loy
akifafanua kwamba katika kampeni hiyo wafanyabiashara hupewa elimu kuhusu
umuhimu wa kusajili biashara zao.
Alisema kampeni
hiyo imefanyika Geita, Simiyu, Mwanza, Mara, Mbeya, Songwe na Rukwa ambako
wafanyabiashara wamekuwa wakitoa ushirikiano mkubwa kwa maofisa wa Brela.
Akizungumzia
usajili wa majina ya biashara, Loy alisema kampeni hiyo ni endelevu kwa nchi
nzima na itaambatana na utoaji elimu kwa wafanyabiashara juu ya muhimu wa
kurasimisha biashara zao na kutambuliwa na mamlaka husika.
Katibu Tawala wa
Mkoa wa Rukwa, Tixon Nzandy alisema ujio wa maofisa wa Brela mkoani mwake ni
fursa ya kuleta mabadiliko ya kiuchumi.
0 comments:
Post a Comment