Mwandishi Wetu, Kigoma
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) linadaiwa kiasi cha
Sh. milioni 41 na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mkoa wa Kigoma, ikiwa ni
malimbikizo ya madeni kutokana na matengenezo ya magari mbalimbali yaliyofanywa
na shirika hilo mkoani humo.
Meneja wa Temesa, Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Hassan Karonda
alitoa madai hayo alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa Mtendaji Mkuu
wa Temesa, Dk. Mussa Mgwatu alipotembelea kituoni hapo.
Meneja huyo ameeleza kuwa kwa sasa Temesa Kigoma ipo
katika operesheni ya kukusanya madeni kutoka kwa taasisi na kampuni inazozidai.
“Mtendaji Mkuu tunazidai Taasisi mbalimbali kiwemo
Shirika la Umeme Tanzania Tanesco, Sh. million 41 hadi sasa,” alisema Mhandisi
Karonda.
Hata hivyo Dk. Mgwatu alimtaka Mhandisi Karonda
kuhakikisha kuwa anakusanya madeni yote anayodai mkoani humo haraka
iwezekanavyo.
“ Fuatilia ofisi kwa ofisi kukusanya madeni ili
kukiwezesha kituo hiki kufanya kazi zake kwa ufanisi mkubwa,” alisisitiza Dk.
Mgwatu.
Akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo Dkt. Mgwatu pia
alipata fursa ya kutembelea kivuko cha MV. Malagarasi na kuona utendaji
kazi wake.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Temesa, Dk.
Mussa Mgwatu yupo katika ziara ya kutembelea vituo vya wakala hiyo nchi nzima
kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo.
0 comments:
Post a Comment