Dk John Magufuli |
Akizungumza jana Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania
(CHAVITA) Mkoa wa Tanga, David Nyange alisema makundi hayo yamesahaulika na kukosa
nafasi za ajira na ruzuku za Serikali.
Alisema Chavita imesahaulika licha ya kutambuliwa na Serikali
na kumtaka Rais awatembelee kujua namna wanavyokabiliana na changamoto za
ukosefu wa ajira na kusababisha kutegemea wafadhili kuendesha maisha yao.
Nyange alisema walemavu wengi wanakabiliwa na changamoto
kubwa ya ukosefu wa ajira kwa kudharauliwa kwenye halmashauri kutokana na
mtizamo hasi ambao unasababisha kuonekana wao si kitu kwenye jamii
hivyo kushindwa kupata ajira hususan kwenye taasisi za umma na binafsi.
‘’Tunamwomba Rais wetu atembelee makundi ya watu maalumu
wenye ulemavu wa kutosikia, ili wamweleze atunge sheria yenye meno makali itakayotulinda
na kuhakikisha tunapata ajira na mikopo ikiwamo ruzuku kama watu wengine,” alisema
Nyange.
Akifafanua kuhusu ukosefu wa ajira kwa makundi ya watu
wenye ulemavu wa kutosikia, Katibu wa CHAVITA Tanga, Monalisa Athumani alisema
makundi hayo hayapewi kipaumbele ipasavyo kutokana na mitazamo hasi
inayoendelea kuwa donda sugu hivyo kushindwa kunufaika na rasilimali zao na maisha kuwa magumu.
“Makundi ya walemavu hususan viziwi, tumesahaulika sana hali
inayofanya kushindwa kupiga hatua
kimaendeleo kwa kukosa fedha na mafungu kwenye halmashauri, licha ya kupata
ushirikiano lakini huduma zinazohusu makundi hayo kwenye mfuko wa maendeleo ya
jamii hatuzipati,” alisema Nyange.
Aidha, Katibu huyo alilalamikia Serikali kushindwa kutenga
fedha na kuyapa ruzuku makundi ya wenye ulemavu wasiosikia hali
inayosababisha makundi hayo kunyanyasika na kuwa ombaomba mitaani.
0 comments:
Post a Comment