Celina Mathew
Shehe Abubakary Ally |
MIEZI mitano baada ya Rais John Magufuli
kuagiza viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), kuchunguza mali
zao, Kamati Maalumu iliyoundwa na Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar bin
Zubeir kuhakiki mali hizo, imewasilisha taarifa ya awali ikibainisha changamoto
kadhaa.
Akizungumza Dar es Salaam jana wakati akikabidhi
taarifa ya uhakiki huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Shehe Abubakary Ally, alisema wamebaini changamoto
kadhaa, ikiwa ni pamoja na baadhi ya mali kutohakikiwa kutokana na kukosekana
kwa taarifa sahihi kama ni za Baraza hilo.
Alibainisha kuwa jambo hilo
limesababisha uhakiki huo kutofanyika kwa wakati na kuomba kuongezwa muda, ombi
ambao liliridhiwa na Shehe Mkuu.
Julai 6, wakati Rais Magufuli akihutubia
Baraza la Eid El Fitr kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe, alitaka viongozi wa
Bakwata kuhakikisha wanasimamia mali zilizo chini yao ili kuepuka migogoro ya
mara kwa mara.
Kwa agizo hilo, Mufti Zubeir aliunda Tume
ya wajumbe wanane kwa ajili ya kushughulikia masuala mbalimbali ikiwamo
misamaha ya kodi iliyoombwa na Bakwata na taasisi zake.
"Leo (jana) tumekabidhi sehemu ya
mwanzo ya ripoti ya Tume iliyoundwa na Mufti, kwa kweli tumekumbana na
changamoto nyingi kwa kuwa ni kazi kubwa kuhoji, kwa kuwa mali za Bakwata ni
nyingi hivyo tumeongezwa muda ili kuikamilisha," alisema Shehe Ally.
Alisema baadhi ya vitu walivyochunguza
kwenye ripoti hiyo ni mikataba, viwanja, majengo na mali zingine za Baraza,
hivyo baada ya Mufti kuisoma ataeleza kilichojiri kupitia vyombo vya habari.
"Kwa sasa hatuwezi kuzungumzia
kilicho ndani ya ripoti hiyo, maana kiongozi wetu aliyetuagiza bado hajaisoma,
hivyo akishaisoma atawaeleza kilichojiri ndani yake," alisema Mwenyekiti
huyo.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa ripoti
hiyo, Mufti alisema ameipokea na kutokana na unyeti ulio kwenye kazi hiyo
ameamua kuwaongeza muda na kuahidi kuwa ataisoma kisha ataeleza kilichomo.
"Nimepokea ripoti hii, kwa kuwa
sijui kilichomo nikimaliza kuisoma nitafanyia kazi mambo yaliyopendekezwa na Tume
kwa mujibu wa kilichoandikwa," alisema.
0 comments:
Post a Comment