Watu 4 kizimbani kwa mauaji


Bahati Othuman, Hai

WATU wanne akiwamo Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Bomang’ombe, wilayani hapa, Nesphory Shayo (33), wamefikishwa  Mahakama ya Wilaya kwa tuhuma za mauji ya mtu waliyemtuhumu kujihusisha na wizi. 

Mbele ya Hakimu Mkazi Agnesi Mhina jana, washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu.

Watu hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 6 jioni Bomang’ombe   kwa kumpiga na kumsababishia kifo Michael Muro (30) wa mtaa wa Bomani.

Mwendesha mashitaka, Hawa Hamisi aliwataja washitakiwa wengine kuwa ni Invocavit Mushi (50), Idd Makere (38) na Yetio Massawe (67) wakazi wa Bomani. Kesi hiyo iliiarishwa hadi Novemba 24 itakapotajwa.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo