Suleiman Msuya
Profesa Makame Mbaraw |
TANZANIA imesema ipo tayari kushirikiana
na nchi mbalimbali kukuza sekta ya usafirishaji katika kutekeleza lengo la
Mandeleo Endelevu Duniani (SDGs) kivitendo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wakati akiwasilisha hotuba yake
mbele wa Wajumbe wa Mkutano wa Dunia kuhusu maendeleo endelevu katika sekta ua
usafirishaji uliofanyika Ashgabat nchini Turkmestan.
Mbarawa alisema historia inaonesha kuwa
usafiri ni njia ambayo inaendesha biashara, uchumi, kazi na maendeleo ya nchi,
hivyo Tanzania imekuwa katika mikakati mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo.
“Kwa sasa inabakia kuwa kiungo muhimu
katika kuunganisha jamii na mipango endelevu, kwani usafiri wa kisasa unaleta
ushindani na unatakiwa kuwa rafiki wa mazingira,” alisema.
Alisema sekta ya usafiri inaunganisha
watu, huduma, uzalishaji na bidhaa kati ya nchi na nchi na dunia kwa ujumla.
Waziri Mbarawa alisema kuwa mwaka 2016 ni muhimu katika kufanikisha
malengo ya SDGs 2030 kupitia usafiri katika kuondoa umasikini, kuboresha afya,
miji na jamii.
Alisema jopo la wataalamu lilitoa
taarifa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Oktoba 28 mwaka huu
wakionesha mchango wa sekta ya usafirishaji katika kutekeleza SDG.
Waziri huyo alisema ili kufanikisha SDGs,
Serikali inapaswa kuwekeza katika mfumo wa usafirishaji barabarani, majini,
anga na maeneo yote yanayohusika ili kuongeza ubora wa maisha.
Alisema sekta ya usafiri inatakiwa kuwa
tayari katika kuleta mapinduzi ya nne ya viwanda ili uzalishaji, huduma na
teknolojia vinaenda kwa pamoja.
“Tunapaswa kutumia njia zote za
usafirishaji kufanikisha usalama wa watu kusafirisha bidhaa, watu na
mawasiliano kwa kanda zote,” alisema.
Waziri Mbarawa alimuwasilisha Rais John
Magufuli katika mkutano huo uliondaliwa na UN katika kujadili nafasi ya sekta
ya usafiri katika SDGs 2030.
0 comments:
Post a Comment