Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya ujenzi
ya China (CCECC), inayojenga barabara ya Magole-Turiani mkoani Morogoro, imeahidi
kukamilisha ujenzi huo mapema, huku ikiiomba Serikali iiunge mkono kufanikisha
azma hiyo kwa kutoa fedha kwa wakati.
Ahadi hiyo ilitolewa
jana na Katibu Mkuu wa Asasi ya Urafiki wa Tanzania na China, Joseph Kahama,
aliyeeleza kwamba siku za nyuma Serikali ilikuwa ikichelewa kutoa fedha
za ujenzi wa miradi na kusababisha kusimama mara kwa mara.
“Nina matumaini
makubwa ya ujenzi kukamilika kwa muda mwafaka, kuna mawasilianao ya mara kwa
mara kati yetu na TanRoads, pia tayari Serikali imetoa Sh bilioni 41.8, kati ya
Sh bilioni 66.7 zinazotarajiwa kujenga barabara hii,” alisema Kahama.
Alisema hakuna siku
mpya ya kukamilisha kazi hiyo iliyokubaliwa na kwamba wafanyakazi wana ari ya
kazi ya kukamilisha mradi mapema, iwapo Serikali itatoa fedha muda mwafaka,
lakini kasi ya ujenzi itadorora kama fedha hazitapatikana kwa wakati.
Hivi karibuni
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe amekaririwa katika vyombo vya habari
akimhimiza mkandarasi huyo kukamilisha kazi kabla au ifikapo Septemba mwakani.
Kahama alisema Dk
Kebwe alijionea hali halisi ya ujenzi wa barabara na kuhakikishiwa na
Mhandisi Khatibu Khamis, kwamba kazi itakamilika muda mwafaka kwani
hakuna tatizo la vifaa au wafanyakazi.
Barabara ya Mikumi-Mzina
inaunganisha Tanga na mikoa ya Morogoro na Dodoma.
0 comments:
Post a Comment