Abraham Ntambara
Wilfred Lwakatare |
WAZIRI
Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare, amesema hakuridhishwa na utaratibu uliotumiwa na Serikali kushughulikia
suala la waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Kinachomkera
ni kuelekeza michango yote kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Akazungumza
juzi kwenye kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na ITV, Lwakatare alisema Serikali
ilitakiwa kuainisha misaada iliyostahili kupitia kwa Mkuu wa Mkoa na ambayo ingepelekwa
moja kwa moja kwa wananchi.
“Mimi
niliguswa na tatizo hili na pia nilikuwa wa kwanza kuutilia shaka utaratibu
huo. Kweli awali Serikali ilikuwa na nia njema, lakini ilitakiwa iache mianya mingine
ya kusaidia wahanga,” alisema Lwakatare.
Alisema
Serikali ilitakiwa kuwa na mtazamo wa mbali kwanza wa kuangalia sehemu
iliyoathirika ambao ni wananchi badala ya kwenda moja kwa moja kwa Mkuu wa Mkoa.
Alisema
katika kushughulikia suala hilo, alitoa ushirikiano mkubwa kwa Mkuu wa Mkoa na
kubainisha kuwa baada ya Serikali kutoa
masharti magumu kwa wahanga hao kwamba waanze kujihudumia, aligawa maturubai na
mablanketi kwa wahanga.
Mbunge
huyo alisema pia alitafuta wadau wakiwamo wabunge ili wasaidie kutoa misaada ya kuhudumia wananchi wa Kagera
na kwa kuona kuwa kama angechangisha fedha, kungeleta shida, alitafuta
mfanyabiashara wa kusambaza huduma.
Alisema
wadau ambao aliwatafuta alitaka wafike kwa mfanyabiashara huyo na kulipia fedha
za vitu ambavyo wangependa kuvitoa kama mchango, ili mfanyabiashara huyo
avichukue na kuvisambaza kwa waathirika.
Alifafanua
kuwa utaratibu huo ulikumbwa na vikwazo kutokana na kwamba Jeshi la Polisi Kagera
lilikamata mfanyabiashara huyo kwa kutoa huduma hiyo, lakini Lwakatare baada ya
kwenda kutoa ufafanuzi, aliachwa kwani alionekana hana tatizo na kuendelea kutoa
huduma hadi mzigo ulipokwisha.
Akizungumzia
migogoro ya ardhi inayoendelea nchini kwa nafasi yake ya Waziri Kivuli, alisema
tatizo kubwa ni mfumo ambao haukuainisha maeneo kulingana na matumizi.
Lwakatare
alimpongeza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
kwa juhudi ambazo amekuwa akifanya kutatua migogoro na kwamba amepiga hatua
nzuri baada ya kufanya upimaji wa ardhi katika mkoa wa Morogoro.
Aidha,
alimtaka Waziri huyo hata kama bajeti aliyopewa ni ndogo, lakini ahakikishe
anaiwekeza katika upimaji huo wa ardhi ili kupata suluhisho la kudumu kwa
tatizo hilo la ardhi nchini.
Alisema
kama yeye angekuwa Waziri kamili angehakikisha kila senti anayopata kwenye
Wizara hiyo anaielekeza kupima ardhi kwa kuwa ndilo ambalo litafanya kuondokana
na migogoro ya ardhi nchini.
Lwakatare
aliishauri Serikali kushughulikia waliosababisha kwa makusudi migogoro kwa kupokea rushwa na kugawa ardhi zaidi
ya mara moja na kwa kuwa wana mali basi zitaifishwe.
0 comments:
Post a Comment