*Majina ya wadaiwa kuanikwa hadharani
*Trilioni 3/- zakopeshwa tangu mwaka
1995
Peter Akaro
Abdul Badru |
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya
Juu (HESLB), imetoa notisi ya siku 30 kwa wadaiwa wote sugu 142,470 kulipa
kiasi chote wanachodaiwa kinachofikia Sh bilioni 2.3.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Abdul
Badru, alisema jana Dar es Salaam kuwa deni hilo ni la kuanzia mwaka wa masomo
1994/95.
Alisema wanufaika wa mikopo hiyo 93,500
walipelekewa ankara za madeni na kati yao wanufaika 81,055 wanaendelea kulipa
na wengine 12,445 hawajaanza kulipa.
Badru alisema licha ya kutoa notisi hiyo,
watatangaza tena majina ya wadaiwa sugu hadharani ili waajiri, wadhamini wao na
wadau wengine wenye taarifa za wadaiwa hao sugu waziwasilishe kwenye Bodi hiyo.
“Pia tutawasiliana na wadhamini wa
wadaiwa hawa ili wawasilishe taarifa zao au wawalipie madeni yao. Tutawasilisha
majina ya wadaiwa sugu kwenye taasisi zinazotunza taarifa za wakopaji, ili
majina yao yawasilishwe kwenye taasisi zote za fedha kwa ajili kutathimini
tabia zao kabla ya kuwakopesha,” alisema.
Aliongeza kuwa kwa sasa wanakamilisha
taratibu za kuwafikisha mahakamani wadaiwa wote sugu ili walipe madeni yao na
gharama za kuwatafuta na kuendesha kesi.
“Kwa mujibu wa sheria, unapomaliza chuo
unapewa miezi 12 kujipanga kurejesha mkopo, lakini hawa wamevunja utaratibu huo
na kwa kufanya hivyo, wanafanya wengine wakose mikopo,” alisema.
Badru aliongeza kuwa kuanzia Julai 2005
hadi Juni mwaka huu, Bodi ya Mikopo ilitoa zaidi ya Sh trilioni 2.54 kwa
wanafunzi 330,801 na hivyo kufanya jumla ya fedha zilizokopeshwa tangu mwaka 1994/95
hadi 2015/16 kuwa zaidi ya Sh trilioni 2.59.
0 comments:
Post a Comment