Suleiman Msuya
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Simu za
Mikononi ya Vodacom, imetangaza dhamira ya kuuza hisa zake kwa umma na baadaye
kujiunga kwenye Soko la Hisa la Dar es
Salaam (DSE).
Hatua hiyo ni utekelezaji wa Sheria ya Elektroniki na Mawasiliano ya Posta (EPOCA)
na Sheria ya Fedha ya Mwaka 2016 ambayo inaelekeza makampuni ya simu kumilikisha
asilimia 25 ya hisa zake kwa wananchi.
Mkurugenzi mkuu wa Vodacom, Ian Ferrao
alisema “Tunayo furaha kutangaza kuwa tumeanza rasmi mchakato wa kuuza hisa kwa
umma kwa mujibu wa matakwa ya sheria na tumewasilisha maombi na utaratibu mzima
utakaotumika kuuza hisa zetu na ratiba yetu nzima,” alisema.
Alisema utaratibu huo utahusu mchakato kwenye
Mamlaka ya Usimamiaji wa Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na DSE.
0 comments:
Post a Comment