Suleiman Msuya
Israel Kamuzora |
KAMISHNA wa Bima, Israel Kamuzora,
amesema sekta ya bima imejiwekea malengo ya kukua kufikia uchumi wa Sh trilioni
moja mwakani.
Kamuzora alisema hayo wakati akizungumza
kwenye maadhimisho ya Miaka 50 ya Bima nchini, kwamba malengo hayo yatawezekana
kama watafikisha elimu ya bima kwa wananchi wote.
Kamishna huyo alisema wana mikakati ya
kukuza soko la bima kutoka zaidi ya Sh bilioni 400 za sasa hadi Sh trilioni
moja mwakani.
“Tunajipanga kwa kila njia ili kufikia
wananchi wengi ili kujua mambo ya bima nadhani tutafanikiwa,” alisema.
Kamishna huyo alisema mkutano huo wa
bima wa mwaka unawapa fursa wadau kujadili mambo yaliyofanyika mwaka uliopita na
kubaini kilichofanyika vizuri.
"Mtaji wa sekta hii kwa sasa ni
zaidi ya Sh bilioni 450 fedha ambazo sekta hii imewekeza, lakini pato lake ni
Sh bilioni 650 na tunatarajia mwakani kufika Sh trilioni moja," alisema.
Alisema jamii inapaswa kujua umuhimu wa
bima na hata tetemeko lililotokea Kagera lisingeleta malumbano ya misaada kama
wananchi wangekuwa wamejikatia bima.
Naibu Katibu Mkuu Utumishi, Suzan Mlawi
akifungua mkutano huo, alisema wakati uchumi wa nchi ukikua, kumekuwa na
ongezeko kubwa la mahitaji ya bima katika sekta mbalimbali kama za viwanda,
kilimo nakadhalika.
"Sekta hiyo imekuwa ikichangia kwa
mwaka uchumi kwa asilimia 16, sekta pia imekuwa ikiondoa hatari ambayo
wangeipata watu au wafanyabiashara katika maisha yao ya uwekezaji," alisema.
Alizitaja changamoto zinazoikabili sekta
hiyo kuwa ni pamoja na masoko na elimu
finyu juu ya bima, ambapo alisema kampuni nyingi za bima zimelenga watu wa
chini na si kampuni kubwa zinazochangia pato kubwa kwa Serikali.
0 comments:
Post a Comment