Lipumba: Maalim Seif hajui atendalo


Warioba Igombe, Morogoro


MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesisitiza kwamba hana ugomvi na katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad akiamini kuwa katibu huyo hajui alitendalo.

Akizungumza na wanachama wa chama hicho wanaomuunga mkono mkoani Morogoro, Profesa Lipumba alisema anatamani kuona Maalim Seif anaacha tofauti zake naye na kurudi ofisini ili wafanye kazi pamoja.

CUF imekuwa katika mgogoro kwa muda sasa ikipasuka makundi mawili;  kundi linalomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba na lingine linalomuunga mkono Maalim Seif Sharif Hamad.

Alisema baada ya kujiudhuru wadhifa wake, CUF iliyumba ndiyo maana CCM ikapata mwanya wa kuchukua madaraka kwa nguvu kutumia njia ya kurudia uchaguzi.

“Kwa muda wote niliokuwa nje ya chama mambo mengi ya ovyo yalifanyika yaliyosababisha kule Zanzibar mgombea wetu akanyang’anywa ushindi wa urais kwa nguvu sasa nimeamua kurudi kundini ili kurudisha heshima,”alisema Lipumba.

Lipumba alimtupia lawama Maalim Seif akisema chama hicho kimekuwa kikiyumbishwa naye kwa kueneza propaganda nyingi juu yake zilizosababisha baadhi ya wanachama kwenda mahakamani.

Hata hivyo profesa Lipumba alisema kuwa yeye amemsamehe kiongozi huyo mwandamizi.

“Baadhi ya wanachama wa CUFwamekwenda mahakamani kupinga mimi kurudi kwenye kiti changu, hii inasababishwa na propaganda za Maalim Seif, lakini mimi sina kinyongo naye pamoja na wananchi wa Zanzibar,” alisema Lipumba.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Magdalena Sakaya amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kuacha kuingilia mambo yasiyowahusu ndani ya chama hicho, akisema kufanya hivyo ni kuzidi kuivurauga CUF na kuwagawa wanachama.

Baadhi ya wanachama wa CUF wamempongeza Profesa Lipumba kwa uamuzi wake wa kurudi kwenye wadhifa wake wakiahidi kuendelea kumuunga mkono ili aweze kurudisha hadhi ya chama hicho.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo