Mwandishi Wetu
WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) unatarajia kujenga
maghorofa matano ya ghorofa nane hadi tisa kila moja katika awamu ya kwanza ya
ujenzi wa nyumba za makazi Magomeni Kota, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Ushauri wa TBA, Edwin Nnunduma alisema hayo
jana wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kukagua ujenzi huo katika
eneo hilo.
Awali Majaliwa alitaka wataalamu wa ujenzi wa mradi wa
nyumba za makazi Magomeni watumie utaalamu wao vizuri wakamilishe ujenzi huo
kwa wakati.
Waziri Mkuu alitaka wataalamu hao waendelee kufanya kazi
hiyo kwa kufuata misingi ya weledi wa taaluma yao, kwani Serikali inawaamini.
“Muhimu mjue kwamba mmepewa dhamana hii kubwa ya
kukamilisha ujenzi huu, ili wananchi waliokuwa wanaishi hapa warudi kwenye
makazi yao,” alisema.
Nnunduma katika maelezo yake, alifafanua kuwa awamu ya
kwanza ya ujenzi huo itahusisha majengo matano.
“Kati ya majengo haya, manne yatakuwa na ghorofa nane na
moja ghorofa tisa, ambapo wakazi zaidi ya 600
waliokuwa eneo hili tangu zamani watakabidhiwa,” alisema.
0 comments:
Post a Comment