Mwandishi Wetu
Profesa Mohamed Bakari |
MGANGA Mkuu wa
Serikali, Profesa Mohamed Bakari, ametaka watoa huduma za afya nchini kufanya
kazi kwa bidii na kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
Profesa Bakari
alitoa kauli hiyo wakati akifungua kongamano la siku tatu la Chama cha
Wafiziotherapia Tanzania (APTA) juzi Dar es Salaam.
“Mnatakiwa kuwa
na nidhamu na kuhudumia vizuri wagonjwa. Fanyeni kazi kwa bidii kwani nchini
kuna mabadiliko makubwa ya kiutendaji,” alisema Profesa Bakari.
Aliwataka kuzingatia
maadili ya kazi kwani Serikali ya sasa inataka watumishi wa umma kufanya kazi
kwa bidii ili kuongeza uzalishaji na kutoa huduma bora katika maeneo yao ya
kazi.
Kongamano hilo
lilikutanisha wataalamu wa afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),
Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC) na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF).
0 comments:
Post a Comment