Peter Akaro
Rais John Magufuli |
UMOJA wa Maaskofu wa Kipentecoste
Tanzania (UMKT) umetoa msimamo juu ya mgogoro kati yao na Baraza la Makanisa ya
Kipentecoste Tanzania (CPCT) ukimwomba Rais John Magufuli na Askofu Sylvester Gamanywa
kuingilia kati kabla ya kufikishana mahakamani.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa
juzi na Mwenyekiti wa UMKT, Askofu Pius Ikongo ilieleza kuwa sheria inataka
kabla ya madhehebu au taasisi za kidini kufikishana mahakamani, ni vizuri
kutanguliwa na usuluhisho na wameshakwenda mahakamani kushauri hilo.
“Hatukubaliani na kitendo cha kufutwa kwa
Baraza na kutumika Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi kulazimisha madhehebu ya kipentecoste kuwa wanachama wa CPCT,”
ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Pia walipinga kitendo cha Ofisi ya Msajili
wa Vyama vya Kijamii kulazimisha wateja wake wanaokwenda kwao kupata huduma za usajili
kutambuliwa na CPCT kwanza na kulipa Sh 200,000 kuwa mwanachama.
“Hatukubaliani na uongozi wa CPCT
kuwakataa na kuwaondoa maaskofu kwenye nafasi zote za uongozi kitaifa, kimikoa,
kiwilaya na kuwaweka wachungaji kuwa viongozi na watatuzi wa migogoro ya madhehebu
ya kipentecoste Tanzania,” ilisema.
0 comments:
Post a Comment