Leonce Zimbandu
MVUA zinazonyesha Dar es Salaam zimesababisha
uharibifu wa miundombinu ya barabara, madaraja na baadhi ya huduma za kijamii
kusimama katika maeneo mbaloimbali.
JAMBO LEO jana ilitembelea Buguruni
Malapa, bonde la Mto Msimbazi, barabara ya Kawawa, Mikocheni, Kawe na
kushuhudia maji barabarani, mitaroni na baadhi ya maduka kufungwa na wananchi
kushindwa kuendelea na biashara zao.
Wakati mvua hiyo ikinyesha abiria walijificha kwenye vituo vya daladala, huku baadhi
wakishindwa kupanda wala kushuka vituoni
kutokana na maji kujaa barabarani.
Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya wakazi
wa maeneo yaliyoathirika, walisema mvua hiyo inaweza sababisha maafa hasa kwa
wakazi wa mabondeni ambao walishindwa kuchukua hatua ya kuhama.
Mkazi wa Buguruni, John Mkalamba alisema
huu ni msimu wa mvua, hivyo wanaoishi maeneo hatarishi wanapaswa kuchukua
hadhari na kuondoka.
Alisema mvua ya siku moja tu imesababisha
madhara haieleweki kama itaendelea kunyeshwa kwa kiwango gani, kwani hali ya
miundombinu si nzuri.
“Huu ni msimu wa mvua hivyo kutokana na
miundombinu mibovu mafuriko yanaweza kutokea, kwani mvua ya siku moja baadhi ya
magari yameshindwa kutembea barabarani,” alisema.
Mwelekeo wa mvua za vuli katika kipindi cha Novemba,
kulitarajiwa na upungufu wa mvua katika maeneo mengi ya nchi
katika kipindi hicho.
Taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilisema maeneo
ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki na maeneo ya mkoa wa Tabora mvua zilitarajiwa
kunyesha katika wiki ya tatu za Novemba.
Iliendelea kusema kuwa mvua za wastani hadi chini ya wastani
zilitarajiwa katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria na mvua za
chini ya wastani katika maeneo mengine ya nchi.
0 comments:
Post a Comment