Mary Mtuka
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amezindua Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la
Reli Tanzania (TRL) na kuisainisha mkataba wa makubaliano ya kazi.
Aidha amewaonya wajumbe hao wa bodi kuwa yeyote atakaye kwenda kinyume na
makubaliano hayo atafukuza kwenye bodi hiyo.
Akizungumza baada ya halfa hiyo Waziri
Mbarawa alisema hatasita kumuengua mjumbe yeyote wa bodi hiyo atakayeshindwa
kuonesha utendaji kazi ulio bora.
Aliwataja wajumbe hao kuwa ni Profesa
John Kandolo ambaye ni Mwenyekiti, Mhandisi Charles Muvungi, Mahamudi Mashaka,
Linfold Mboma na Matha Maida.
"Kuzinduliwa kwa bodi hii kumekuja
mara baada ya shirika kukaa bila bodi kwa
zaidi ya mwaka tangu bodi hiyo ilipovunjwa Septemba 2015," alisema
Prof.Mbarawa
Aidha alisema kuwa Serikali imejipanga
kufufua usafiri wa reli ili kurahisisha usafiri na kupunguza ajali za
barabarani.
"Lengo ni kuhakikisha tunapunguza ajali za barabarani pamoja na
kuzilinda barabara ilivzidumu kwa muda mrefu," alisema Prof. Mbarawa.
Alisema tayari zabuni ya Dar es salaam-
Morogoro ilishatangazwa na wakandarasi zaidi ya 40 wameomba zabuni hiyo ambayo
itafunguliwa Desemba 6 mwaka huu.
Aliongeza kuwa treni hiyo itakuwa ya
kisasa yenye uwezo wa kukimbia kwa speedi zaidi ya 120 hadi 160 tofauti na
ilivyokuwa awali.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo,
Masanja Kadogosa alisema wanaamini kupatikana kwa bodi hiyo mpya kutasaidia shirika
kufanya maamuzi kwa haraka.
Alisema hapo awali ilikuwa ni vigumu
kufanya maauzi ya kiutendaji ndani ya shirika bila kupitia bodi ya wakurugenzi.
"Kwa niaba ya shirika la reli ninaaidi
kutoa ushirikiano kwa bodi katika masuala ya uwendeshaji na usimazi wa majukumu
ya kampuni," alisema.
Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo Profesa
John Kandoro alitumia fursa hiyo kushukuru na kuomba ushirikiano kutoka kwa
wafanyakazi na uwongozi kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment