Salha Mohamed
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela,
amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kutokana na maradhi.
Mkuu huyo alipokewa hospitalini hapo
juzi na kulazwa katika wodi ya Sewa Haji chumba namba 18.
Akizungumza Dar es Salaam jana Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa MNH, Aminiel Aligaesha alisema Shigela
alipokewa saa 12 jioni.
“Tulimpokea jana (juzi) saa 12 jioni na
kumpa huduma ya matibabu lakini kwa sasa afya yake imeimarika,” alisema.
Alisema awali walimpokea akiwa na hali
mbaya lakini kutokana na juhudi za madaktari alitibiwa na afya yake imeimarika
na anaendelea vizuri.
0 comments:
Post a Comment