Peter Kimath, Mlimba
Freeman Mbowe |
CHADEMA imetangaza
mpango wa kuacha kutegemea ruzuku ya vyama vya siasa kutoka Serikali Kuu kwa
kuanza kutoa kadi za uanachama kwa mfumo wa elektroniki utakaoiingizia mapato makubwa.
Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe, alibainisha hayo juzi kwenye mkutano na watendaji
wa chama hicho jimboni Mlimba, wilayani Kilombero ukihusisha viongozi wa chama
hicho ngazi za vitongoji, vijiji, kata na wabunge.
Alisema ifikapo
mwakani, chama kitaanza rasmi kutumia kadi za elektroniki kwa wanachama wake
badala ya zile za zamani kwa lengo la kutumia kadi hizo kama chanzo kikuu cha
mapato.
"Tutakapoanza
kutumia mfumo huo wa kadi za elektroniki utawezesha wanachama kunufaika na
mapato yatakayotokana na uuzaji wa kadi hizo badala ya kutegemea ruzuku pekee
kuendesha chama,’’ alisema Mbowe.
Alisema fedha
zitakazokusanywa kutokana na mauzo hayo hazitakwenda Taifa na badala yake
zitakwenda ngazi husika hususan kwenye majimbo ili kutumika kwa shughuli
mbalimbali ikiwamo kujenga ofisi za chama, vifaa vya uenezi na masuala mengine.
Mbunge wa Mlimba
ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa, Suzan Kiwanga alisema kumekuwa na
kuzorota kwa ununuzi wa kulipia ada za uanachama na hivyo chama kukosa mapato
na kutaka wanachama kuchangamkia kununua kadi hizo mpya pindi mchakato
utakapokamilika.
Kiwanga alisema
uongozi wa CHADEMA umebadilisha mfumo wa utoaji kadi kwa kuweka progamu maalumu
ya kutambua wanachama wake nchi nzima kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2020.
Mkazi wa Mlimba,
Renatus Shija, alisema kukamilika kwa mfumo huo kutawezesha wanachama kuwa na
kadi za uhakika ambazo zitawawezesha kutambulika na kuuomba uongozi wa kitaifa
kuwajengea uwezo kwa kufanya vikao vya ndani.
0 comments:
Post a Comment