Mery Kitosio, Arusha
SERIKALI ya
Ujerumani kupitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) imetoa msaada wa euro
milioni 30 (Sh bilioni 60) kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ili
kutoa chanjo kwa watoto wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
Mbali na msaada
huo wa chanjo, Serikali pia imetoa euro milioni 10 kwa ajili ya kuwekeza kwenye
maabara ya watoto ili kuhakikisha magonjwa ya watoto yanatokomezwa kwa wakati.
Akizungumza
katika hafla fupi ya kusaini mkataba wa fedha hizo katika makao makuu ya
jumuiya hiyo juzi, Balozi wa Ujerumani ambae pia ni Mwakilishi wa Benki hiyo,
Egon Kochanke alisema kutolewa kwa msaada huo wa fedha kutapunguza magonjwa ya
watoto.
Alisema fedha
hizo zitahudumia watoto wote wa Jumuiya kwa kuwapa chanjo za kukinga magonjwa
na pia kupunguza matatizo kwenye sekta ya afya ya upungufu wa dawa hasa za
watoto.
"Serikali
yetu ya Ujerumani leo hii tumesaini mkataba na Jumuiya hii ya Afrika Mashariki
na tumetoa Sh milioni 60 za maabara ili kutoa chanjo ya watoto kwenye
sekta ya afya.
“Lengo letu ni
kuhakikisha wanapata huduma za kiafya, kuanzia wanapozaliwa si watoto
wanapelekwa kupata chanjo wanaambiwa zimekwisha," alisema.
Akielezea msaada
wa fedha hizo za maabara ya watoto, alieleza kuwa kuwepo kwa maabara hiyo
kutapunguza magonjwa yanayopata watoto, kwani itakuwa ni maabara ambayo ni
maalumu tu kwa ajili ya kupambana na udhibiti wa magonjwa ya watoto wa nchi za
Jumuiya.
Akizungumza
baada ya kumaliza kusaini mkataba wa fedha hizo, Katibu Mkuu wa EAC, Liberat
Mfumukeko aliishukuru Serikali ya Ujerumani kwa misaada hiyo, ambayo wamekuwa
wakiitoa kwa Jumuiya hiyo na kusema kuwa itapunguza changamoto za afya hasa
kukabiliana na vifo vya watoto.
Mfumumeko
alisema fedha hizo ambazo zinalenga kusaidia watoto wote wa Jumuiya
atahakikisha zinafikia walengwa, huku akiangalia zaidi zile nchi ambazo zina mahitaji
makubwa ya kutibu chanjo hizo.
0 comments:
Post a Comment