Grace Gurisha
Biswalo Mganga |
MKURUGENZI
wa Mashitaka (DPP), Biswalo Mganga, amekata rufaa dhidi ya maofisa wawili wa Ofisi
ya Waziri Mkuu kitengo cha Mpigachapa Mkuu wa Serikali, wanaodaiwa kughushi kiapo
cha cheti cha ndoa na cha kuzaliwa.
Hatua
hiyo imefikiwa baada ya Mahakama ya Wilaya ya Temeke kuwaacha huru kwa madai
kuwa hakuna ushahidi utakaowasababisha wajitetee.
Maofisa
hao ni Edwin Igenge na Stella Ndomba, ambao walikuwa wanashitakiwa kwa makosa
12 ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo, kujiwasilisha isivyo halali na
kukutwa na nyaraka ambazo kisheria hawakupaswa kuwa nazo.
Baada ya
hatua hiyo, DPP alionesha kutokuridhika na uamuzi wa Aprili 27 wa Hakimu Mkazi,
Godfrey Mwambapa wa Mahakama hiyo, hivyo kuamua kukata rufaa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kupinga washitakiwa hao kuachwa huru pasipo
kujitetea.
Katika
uamuzi wake, Hakimu Mwambapa alisema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi wanane
washitakiwa hawana kesi ya kujibu na kwenda mbali zaidi kuwa ushahidi
uliotolewa ni dhaifu kuwataka maofisa hao wajitetee.
Pia
alisema katika baadhi ya mashitaka, upande wa mashitaka ulishindwa kuleta
shahidi hata mmoja wa kuzungumzia hali hiyo hivyo akawaacha huru.
Katika mashitaka
ya kwanza Igenge alidaiwa kuwa Julai mosi 2009 na Novemba 3, 2009 kwa nia ya
kudanganya, alijiwasilisha kwa Mary Nangale, Esther Ashery kuwa yeye ni wakili na Kamishna wa viapo, huku kwa
kuidhinisha hati zao wakati akijua hana mamlaka hayo.
Igenge
alishitakiwa kuwa Juni 2009 kwa nia ya kudanganya, alighushi na kuwasilisha
waraka wa Januari 2, 2008 ambao ni fomu za viapo kwa Salome Kapongo na Zakayo
Magesa kuonesha kuwa hati hizo zilikuwa halali.
Pia
anadaiwa kuwa aliwasilisha cheti cha kuzaliwa namba 00176894, cheti cha ndoa
namba 00577939 kwa Katibu Mkuu, ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Mpichachapa
Mkuu wa Serikali kwa manufaa binafsi
Katika mashitaka
ya 12 Igenge alidaiwa kuwa Machi 5, 2012 akiwa Ubungo
Kibangu alikutwa na nyaraka za ofisi yakiwamo maombi ya kukabidhiwa bunduki
tano za kuzuia wanyama wahalifu na kuua mbwa na paka na maombi ya Wizara kuhusu
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na CBRT wakati akijua kuwa hana mamlaka
hayo.
0 comments:
Post a Comment