Leonce Zimbandu
IGP Mangu |
RAIA wa Uturuki, Erhan Copkur (24)
ameuawa kwa kupigwa risasi tatu na watu wawili wasiojulikana na kumpora begi
dogo jeusi.
Mauaji hayo yalifanyika juzi saa nane
mchana kwenye mataa ya Superstar barabara ya Sam Nujoma, Kinondoni, Dar es
Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni,
Suzan Kaganda alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na gazeti hili.
Alisema wauaji hao waliokuwa kwenye pikipiki
mbili nyeusi aina ya Boxer ambazo namba zake hazijajulikana, walimvamia na
kumpiga risasi hizo na kumpora begi.
“Tunaendelea kuwasaka waliohusika na
tukio hilo, kwani hadi sasa hakuna aliyekamatwa,” alisema.
Mmoja wa mashuhuda wa mauaji hayo ambaye
hakupenda kutajwa jina kwa sababu za kiusalama, alidai waliona pikipiki hizo
zikifukuzana lakini hawakujua kuwa ni majambazi.
Kwa mujibu wa madai ya shuhuda huyo, baada
ya watu hao kufika eneo hilo la Superstar, walisikia milio ya risasi na hakukuwa
na raia hata mmoja aliyekwenda kushuhudia.
“Tulifika eneo hilo baada ya wenye pikipiki
hizo kuondoka, inawezekana lile begi jeusi lilikuwa na fedha kwani haiwezekani
majambazi watumie nguvu ile bure,” alisema.
Alisema kama mhusika aliporwa fedha
wakati mwingine ni uzembe kwani si vizuri kutembea na fedha nyingi kwenye begi
bila ulinzi wa aina yoyote.
0 comments:
Post a Comment