Joyce Kasiki, Dodoma
Hussein Bashe |
SERIKALI imesema inaendelea kutekeleza miradi ya
kufikisha umeme katika maeneo yote ya vijijini ikiwa ni pamoja na katika vijiji
vya Nzega Mjini.
Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa
Nishati na Madini Medard Kalemani alipokuwa akijibu swali la Nyongeza la Mbunge
wa Nzega Mjini Husein Bashe (CCM).
Katika swali lake Bashe (pichani) alitaka kujua ni lini
Serikali itapeleka umeme wa REA awamu ya tatu katika jimbo hilo.
“Naomba kujua ni lini Serikali itapaeleka umeme katika
vijiji vya Mwanzole, Bulunde na Kashishi,” alihoji Bashe Akijibu Kalemani
alisema, Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya kufikisha umeme katika maeneo
yote ya vijijini nchini ikiwemo katika Jimbo la Nzega Mjini kupitia mradi wa
REA awamu ya tatu.
Awali akijibu swali la msingi la Mbunge wa Mufindi Kusini
(CCM) Mendrad Kigola ambaye alitaka kujua ni lini Serikali itapeleka umeme
katika Kata za Idete,Idunda,Kiyowelo, Maduma na Mtambula ili wananchi waweze
kufaidika na huduma hiyo.
Akijibu Kalemani alisema, Serikali inaendelea kutekeleza
miradi yakufikisha umeme katika maeneo yote nchini ikiwa ni pamoja na vijiji
vya Mufindi Kusini.
Kalemani alisema vijiji vya Kata ya Idete, Idunda,
Kiyowela, Maduma na Mtambula vitapatiwa umeme kupitia mradi wa REA awamu ya
tatu.
Alisema kazi ya kupeleka umeme kwenye vijiji hivyo pamoja
na katika Wilaya ya Mufindi itahusisha ujenzi wa njia ya njia ya umeme, msonga
wa kilovoti 0.4 yenye urefu wa Kilomita 81, ufungaji wa trasfoma 24 pamoja na
kuwaunganishia umeme wateja wa awali 3,533.
0 comments:
Post a Comment