Julius Konala, Nyasa
Simbachawene |
BARAZA la Madiwani
la Halmashauri ya Wilaya limewafukuza kazi watumishi watatu wa halmashauri ya hiyo kutokana na makosa mbalimbali yakiwamo ya
utoro kwenye vituo vyao vya kazi.
Uamuzi huo
ulifikiwa jana kupitia kikao cha Baraza la Madiwani chini ya Mwenyekiti wake, Alto
Komba na kuhudhuriwa na watendaji wa Halmashauri hiyo.
Komba alitaja
watumishi waliosimamishwa kuwa ni John Chota, Fundi Sanifu wa Maabara Daraja la
Pili, Dk Emmanuel Nkumbi na Geofrey Kayombo, Mhasibu Daraja la Kwanza.
Aidha, madiwani
hao walimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyasa, Dk Oscar Mbyuzi
kwa hatua na jitihada anazofanya kuhakikisha anainua uchumi wa Halmashauri hiyo
kimapato na kuwa mstari wa mbele kusimamia makusanyo ya ushuru na kuziba mianya
ya ufujaji wa fedha za Serikali.
Walisema katika
kipindi kifupi tangu ateuliwe na Rais John Magufuli kuwa Mkurugenzi, amekuwa
mstari wa mbele kuhakikisha anainua uchumi wa Halmashauri kwa kutumia fursa
mbalimbali zilizopo wilayani humo.
Waliiomba
Halmashauri hiyo kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa miradi yote viporo kabla ya
kuanza mipya kwa lengo la kuunga mkono nguvu za wananchi ambao wamekuwa mstari
wa mbele kujitolea kwenye maendeleo.
0 comments:
Post a Comment