Dotto Mwaibale
Ummy Mwalimu |
SAKATA la Julieth Daudi (19) mkazi wa
Tabata Relini pamoja na ndugu zake kususia kuchukua mwili wa mtoto
aliyejifungua kwa madai kuwa mtoto huyo hakuwa wake, limechua sura mpya.
Julieth ambaye anaamini kuwa wake
amebadilishwa na wauguzi wa Hospitali ya Amana katika Manispaa ya Ilala jijini
Dar es Salaam baada ya kujifungua sasa amepanga kufikisha suala hilo kwa Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii.
Julieth alisema “tunahitaji kwenda
kumuona Waziri waAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Ummy
Mwalimu, kwa hatua zaidi kutokana na kitendo hicho walichofanyiwa na wauuguzi
hao.”
Aliendelea "Mimi pamoja na ndugu
zangu tutakwenda kumuona waziri ili kumpelekea malalamiko yetu."
Akizungumzia mkasa huo Daudi alisema alifika
Hospitalini hapo Februari 2 jioni akiwa amesindikizwa na mama yake Veronica
Lucas na shangazi yake Judith Christopher.
"Nilipofika daktari aliponipima
aliniambia kuwa hasikii mapigo ya mtoto isipokuwa ya kwangu hivyo alishauri
siku iliyofuata nipate kipimo cha utrasaund lakini kabla ya kipimo hicho
nilijisia uchungu na kujifungua" alisema Daudi.
Daudi alisema baada ya kupita muda
kidogo muuguzi aliyemzalisha alimfuata na kumueleza kuwa mtoto wake alikuwa
amefariki na alipomuuliza alikuwa wa jinsia gani muuguzi huyo alimweleza kuwa
alikuwa hajui kama alikuwa wa kiume au wa kike.
Aliongeza kuwa wakati yupo wodini
alimuona kijana mmoja aliyevalia koti la hospitali akiwa amembeba mtoto ambaye
hakujua alikokuwa amempeleka.
Alisema baada ya kuambiwa mtoto wake
amefariki aliomba aonyeshwe lakini hakuoneshwa tangu saa tatu asubuhi ambapo
alilazimika kwenda kuomba simu kwa mlinzi wa hospitali hiyo na kuwajulisha
ndugu zake walipofika nao waliomba kuonyeshwa mwili wa mtoto huyo bila mafanikio.
Shangazi wa Julieth Judith Christopher
alisema baada ya kutokea tukio hilo walikwenda kumuona Mganga Mkuu wa Hospitali
hiyo ambaye aliitisha kikao baina ya ndugu pamoja na maofisa wengine wa
hospitali hiyo ambacho hakikufikia muafaka baada ya ndugu hao kukataa kuuchukua
mwili wa mtoto huyo wakidai si wa kwao.
Aliongeza kuwa mganga mkuu huyo
aliwaeleza kuwa mtoto huyo alikuwa amefia tumboni baada ya mimba hiyo
kuharibika na ndiyo sababu mtoto huyo alizaliwa akiwa mfu.
"Wanafamilia tumegoma kuuchukua mwili
wa mtoto huyo na maamuzi yaliyofikiwa ni kufanyika kipimo cha DNA" alisema
Christopher.
Alipopigiwa simu na gazeti hili Muuguzi
Mkuu wa Hospitali hiyo, Beauty Mwambebule alisema hawezi kulizungumzia tukio
hilo kwenye simu njia
ya simu badala yake alimtaka mwandishi
wetu kwenda hospitali kupata undani wa jambo hilo.
0 comments:
Post a Comment