Sekta ya mazingira yakabiliwa na ukata


Edith Msuya

January Makamba
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, amesema changamoto inayoikumba sekta ya mazingira kwa sasa ni fedha.

Akizungumza jana Dar es Salaam wakati akizindua Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira, Makamba aliitaka Bodi hiyo kupambana ili kupata fedha ambazo zitasaidia kutunza na kuhifadhi mazingira.

"Mfuko huu ni mpya, hivyo ni jukumu ambalo mnatakiwa kuwa nalo kuhakikisha mnapata fedha ili kufanya mazingira yatunzike na kufanya mfuko huo kukua," alisema.

Makamba alisema ni lazima Bodi iwe na mpango mkakati  wa miaka mitatu  ambao utaukuza mfuko huo na kuondokana na utegemezi ili kutatua mambo mbalimbali ya kimazingira.

Alisema bado kuna changamoto za masuala ya mazingira hasa katika kuhakikisha yanakuwa bora.

"Kwa muda mrefu hapakuwa na mfuko kama huu, hivyo kwa kuwa ndiyo unaanza kazi vipaumbele vyake ni kuhakikisha mazingira yanatunzwa na kutafuta fedha zitakazofanya mfuko huo uendelee," alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo