Diwani ashikiliwa kwa mauaji


Joyce Kasiki, Dodoma


DIWANI wa Zanka, Lista Chilangwa (CCM) anashikiliwa na Polisi wilayani Bahi, kwa tuhuma za kumuua Isaya Bayanga (60), mkazi wa kitongoji cha Mkonghoni kijijini Mkondai.  

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alithibitisha jana kukamatwa kwa Diwani huyo huku akisema yuko mbali na ofisi hivyo asingeweza kulingumzia kirefu.

Lakini Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Danford Chisomi alikiri kupokea barua ya Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Bahi ikieleza Diwani huyo kushikiliwa na Polisi.

Alidai kuwa tetesi zilizopo ni kwamba Diwani huyo alikuwa akidaiana na mzee huyo Sh milioni tatu.

Chisomi alidai kuwa kabla ya tukio hilo, Diwani alimwamuru Mtendaji wa Kata amkamate mzee huyo na kumweka ndani (kwenye ofisi ya kata).
 
Kuhusu maslahi ya Diwani huyo, Chisomi alidai kuwa wanasubiri mchakato wa mahakamani utakavyomalizika ndipo ijulikane kwa kuzingatia sheria zilizopo.
Hata hivyo, alisema kwa upande wa posho za vikao na ya mwezi hatapata kipindi hiki ambacho kesi inaendelea.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio, Lista anadaiwa kutenda kosa hilo mwishoni mwa Januari, lakini polisi hawakumkamata kutokana kutoroka na familia yake, mpaka alipojisalimisha Polisi akakamatwa.

Ilidaiwa kuwa chanzo cha Diwani kudaiwa kutenda kosa
hilo, ni baada ya polisi kufika eneo la tukio na kukuta simu yake imelaliwa na marehemu na kuthibitisha kuwa yake
baada ya kupiga namba za simu hiyo ambazo ziliita.
 
Mwili wa Bayanga uliokotwa saa 12 jioni siku hiyo njiani
ukiwa umechinjwa na kichwa kutenganishwa na kiwiliwili huku pia ukiwa na majeraha mengine mwilini.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo