Leonce Zimbandu
MITO 80 iliyokuwa ikitirisha maji misimu
yote katika wilaya ya Kilombero, ipo hatarini kukauka.
Aliyekuwa Mbunge wa Kilombero, Abdul
Mteketa alisema hayo jana alipozungumza na mwandishi wa gazeti hili na
kulaumu jamii ya wafugaji na wakulima
kwa kuharibu mazingira ya vyanzo vya maji ya mito hiyo.
Mteketa ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Mazingira katika wilaya hiyo, alisema baadhi ya wafugaji wamekuwa wakinywesha
mifungo maji kuharibu na kingo za mito hiyo na vyanzo vyake vya maji, huku
baadhi ya wakulima wakilima kado ya mito hiyo.
Kwa mujibu wa Mteketa, hata baadhi ya viongozi
wa wilaya hizo wasio waaminifu, wamechangia hali hiyo kwa kutoa ruhusa ya
kufanyika kwa uharibifu huo.
Alisema haiwezekani mtu alime kwenye
vyanzo vya maji na mifugo iachiwe izagae hovyo kwenye mabwawa na mito bila kuchukuliwa
hatua madhubuti.
“Naomba viongozi na wananchi wa wilaya
ya Kilombero wawe makini katika utunzaji wa mazingira na vyanzo
vya maji,” alisema.
Alisema kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa
Mazingira, anapaswa kupaza sauti ili hatua madhubuti za kutunza mazingira zichukuliwe
katika Mto Kilombero ambako kunapatikana mnyama aina ya Puku.
Alisema ikiwa juhudi hazitachukuliwa
kudhibiti mifugo na wakulima kando ya kingo za mito hiyo, baada ya miaka kadhaa
Mto Kilombero utakauka na kusababisha jangwa.
Mteketa alisema hata mkoa wa Morogoro kuchaguliwa
kuwa ghala la chakula, kulitokana na bonde la Mto Kilombero, hivyo tahadhari
isipochukuliwa hata jukumu la mkoa huo la kuwa ghala la chakula litashindikana.
0 comments:
Post a Comment