Abraham Ntambara
CHAMA cha ACT- Wazalendo, kinatarajia
kufanya mjadala wa kitaifa katika kuadhimisha miaka 50 ya Azimio la Arusha kutafakari
mafanikio na mapungufu yake katika Tanzania ya leo.
Hayo yalibanishwa jana jijini Dar es
Salaam na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma Ado Shaibu aliyesema
kuwa mkutano huo wa kidemokrasia utafanyika Machi 25 mwaka huu jijini Arusha.
“Mkutano huu wa kidemokrasia, utajadili
nafasi ya siasa za kijamaa na za mlengo wa kushoto barani Afrika na duniani
katika zama hizi za kukua kwa kasi kwa siasa za mlengo wa kulia,” alisema
Shaibu.
Shaibu alisema katika maazimisho hayo,
ACT kitatumia mkutano huo kutafakari dhana na msingi wa Azimio la Tabora
linalohuisha Azimio la Arusha katika mazingira ya karne ya 21.
Aidha alieleza kuwa mbali na viongozi wa
chama hicho mkutano huo utawaaleta pamoja wanasiasa wa vyama mbalimbali,
wawakilishi wa Asasi za Kiraia, wanazuoni na wanaharakati kutoka ndani na nje
ya nchi.
Alisema wamekwishatoa mialiko na kufanya
mazungumzo na vyama vya Labour (Uingereza), Economic Freedom Fighters–EFF
(Afrika ya Kusini), Die Linke (Ujermani), na Syriza (Ugiriki) ili viongozi wao
washiriki na kutoa maada kwenye mjadala huo.
Aliongeza kwamba watawaalika pia
waliokuwa wanachama wa Taasisi ya Ruvuma Development Association (RDA) pamoja
na wananchi wengine wa kawaida walioishi wakati wa Azimio la Arusha na
kushiriki katika kulitekeleza ili watoe uzoefu wao.
Kwa upande mwingine chama hicho
kimemtaka Rais John Magufuli kuongoza nchi kwa kufuata Katiba na Sheria, Shaibu
alisema ni haki ya kila mswananchi kupata wakili wakumtetea mahakamani.
Shaibu alieleza kuwa Katika siku ya
maazimisho ya kilele cha siku ya sheria Rais alikaririwa akisema kwamba waharifu
wakikamatwa na vyombo vya dora washitekiwe upesi huku akitaka pia wakili
atakayejitokeza kumtetea aunganishwe katika kesi.
“Kwa nia njeama kabisa, kama chama cha
siasa hatuwezi kukaa kimya tunao wajibu wa kumkumbusha kuwa nchi hii
inaendeshwa kwa mujibu wa katiba na sheria,” alisema Shaibu.
0 comments:
Post a Comment