Christina Nkya, Dodoma
Kassim Majaliwa |
WAZIRI
Mkuu, Kassim Majaliwa, ametaka wananchi kutumia vizuri mvua zinazonyesha nchini,
kulima mazao ya muda mfupi, ili kukabiliana na uhaba wa chakula katika baadhi
ya maeneo nchini.
Alitoa ushauri
huo juzi alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Magu, Kiswaga Desideri (CCM), katika
kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu.
Desideri
alitaka kujua Serikali inachukua hatua gani kukabiliana na uhaba wa chakula.
Katika
hatua nyingine, Majaliwa alisema Serikali inaendelea kuimarisha viwanda vya
ndani, ili vizalishe sukari kwa wingi kuepuka upungufu wa bidhaa hiyo kama
uliotokea mwaka jana.
Akijibu swali
la Mbunge wa Mvomero, Suleiman Sadik (CCM), Majaliwa alisema Serikali
haitarajii kuwapo upungufu wa sukari nchini kama ilivyokuwa mwaka jana, kwa
sababu viwanda vya ndani vimeanza uzalishaji na vinaendelea kuzalisha.
Katika
swali lake, Sadik alisema mwaka jana nchi ilikumbwa na uhaba wa sukari
uliosababishwa na uzalishaji mdogo wa viwanda vya ndani na kutaka maelezo
kuhusu hatua za Serikali kukabiliana na hilo.
“Napenda
kujua hali ya upatikanaji wa sukari kwa sasa ikoje nchini na Serikali
imejiandaaje kukabiliana na uhaba huo ili usitokee kama mwaka jana,” alisema
Sadik.
Akifafanua
Majaliwa alisema kwa taarifa zilizopo hadi Machi, nchi itakuwa imefikia malengo
ya uzalishaji kwa sababu mwishoni mwa Januari, uzalishaji ulifikia asilimia 86
ya mahitaji.
Hata
hivyo, alibainisha kuwa kukitokea upungufu wa sukari Serikali itachukua hatua
ya kukabiliana nao.
0 comments:
Post a Comment