Mwandishi
Wetu
Yusuf Manji |
NI Yusuf
Manji anayezungumziwa? Hilo ni swali analoweza kujiuliza mtu yeyote
anayemfahamu mfanyabiashara huyo kwa haiba yake na matendo anapozunguzmiwa na
kumhusishan na mambo yaliyo kinyume katika jamii.
Muda
mfupi baada ya kutajwa kuhusishwa na dawa za kulevya na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Manji ameeleza kushtushwa na kitendo hicho, hata kuhoji kama ndiye
anayezungumziwa.
Katika
mahiojiano na gazeti hili Manji alifananisha kutajwa kwake kwenye tuhuma hizo
kuwa ni sawa na mti wenye matunda kupigwa mawe.
Alisema
kuwa licha ya kuunga mkono vita ya dawa za kulevya, utaratibu uliotumika
kumtaja haukubaliki na umemchafua katika jamii aliyoihudumia kwa muda mrefu
“Nimejitoa
kwa mambo mengi kuhakikisha Watanzania wenzangu wanapiga hatua kaitka
maendeleo, ajira, elimu, afya hata michezo na siasa,” alisema.
Alisema
jina lake ni miongoni mwa Watanzania maarufu nchini waliojitoa kwa jamii
kupitia mambo mbalimbali, jina la Yusuf Manji halitowekwa kando.
Hii ni
kutokana na ukweli kwamba Manji (42) amekuwa akijitoa na kujitolea katika
masuala mbalimbali kiuchumi na kijamii hata kuchangia maendeleo ya Taifa
kupitia Kampuni ya Quality Group Limited (QGL) anayoiongoza.
Manji
amekuwa akiongoza QGL yenye biashara takriban 102 katika nchi 28 duniani tangu
akiwa na umri wa miaka 20.
Alipata uongozi huo mwaka 1995, baada ya baba
yake Mehboob Manji kufariki dunia. Mzee Mehboob alikuwa akiendesha kampuni ya
vifaa vya magari.
Tangu
wakati huo, Manji amekuwa akisimamia vyema na kupata mafanikio yaliyowezesha
kuongeza kampuni 17 tangu alipoanza kuongoza kampuni hiyo ameweza kuajiri mamia
ya Watanzania kwenye fani mbalimbali hivyo kuchangia kuboresha maisha ya
Watanzania kwa kipato na pia ukuaji uchumi wa Taifa.
Kampuni
hizo zinajihusisha na biashara ya kimataifa, huduma za vyakula, usambazaji
vyombo vya moto, maendeleo ya makazi na huduma za uchukuzi.
Mfanyabiashara
huyo anetekeleza hayo kukiwa na faida kadhaa za uwekezaji wa ndani kwa taifa.
Moja ya
faida hizo ni kupunguza tatizo la ajira kwa wananchi, kuongezeka kwa bidhaa na
huduma bora kwa wananchi, lakini kubwa fedha na faida za uwekezaji kubaki
nchini.
Tayari
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya RAIS John Magufuli imeeleza kujipanga
kuwasaidia na kuwaunga mkono wawekezaji wote wa ndani, ikiwahakikishia ulinzi
wa viwanda vyao.
Katika moja ya mikutano yake na Shirikisho la Viwanda
Tanzania (CTI) kwa ajili ya utoaji wa Tuzo za Rais kwa wazalishaji bora nchini,
Rais Magufuli ameshamwagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles
Mwijage kuhakikisha anatengeneza mazingira yatakayowapunguzia kodi kwa kiasi
kikubwa wawekezaji wa ndani na kupandisha kodi zaidi kwa bidhaa zinazoingia
kutoka nje ya nchi.
Alisema Tanzania ni nchi yenye utajiri wa rasilimali,
fursa ya masoko, nguvukazi na mazingira mazuri ya uwekezaji, hivyo kipaumbele
kikubwa kitakuwa ni kuhakikisha wazalendo wanapata fursa ya kufungua viwanda
kwa wingi na kutumia ipasavyo fursa hiyo.
Alitaja faida watakazopata wafanyabiashara wa Tanzania endapo
watawekeza na kuanzisha viwanda nchini kuwa ni pamoja na kuongezea Taifa
mapato, kuingiza zaidi fedha za nje na kutengeneza ajira kwa wingi.
Rais aliwataka Watanzania hasa watendaji Serikali na
taasisi zake, kuondokana na tabia ya wivu kwa kuwanyima fursa wawekezaji wa
ndani wanapotaka kuwekeza, badala ya kuwapendelea na kuwaamini zaidi wawekezaji
kutoka nje.
Pamoja
na maelezo hayo kwa haiba, Manji amejipambanua kama mpenda watu hasa vijana kwa
kujihusisha na michezo akiwa Mwenyekiti wa Klabu Kongwe ya Yanga na amekuwa
akijitolea kiasi kikubwa cha fedha kuiendesha.
Mbali na
masuala ya michezo, Manji ni mwanasiasa na Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu, Dar
es Salaam, nafasi aliyoipata katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2015.
Kupitia
wadhifa huo, amekuwa akihudumia wananchi wa kata hiyo katika nyanja tofauti ili
kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa wote kwani lengo la kugombea nafasi hiyo
kwake lilikuwa kuhudumia wakazi hao hasa kuhakikisha wanapata huduma bora.
Manji
ameboresha huduma za afya kwa wakazi hao kwa kujenga hospitali kwenye kata hiyo
ya Mbagala Kuu, kuboresha upatikanaji wa elimu.
Mkurugenzi
Mtendaji huyo wa QG Ltd pia ameanzisha Mpango wa Kutoa Uji kwa wanafunzi wa
shule mbalimbali za kata hiyo hali inayohamasisha watoto kupenda shule lakini
pia kuwa na afya bora.
Mara
kadhaa katika mahojiano na vyombo tofauti vya habari Manji amejipambanua kwamba
nia yake ni kuona Tanzania inasonga mbele na watu wake wanapata maisha bora.
Aliwahi
kueleza kuwa akimaliza kipindi chake cha udiwani nafasi anayotamani kuiwania ni
ujumbe wa nyumba kumi ili kuwatumikia wananchi wa kawaida.
Pia
aliwahi kueleza kwamba ikiwa ataombwa kuwania ubunge, basi atakuwa tayari
kufanya hivyo katika majibo yenye umasikini mkubwa ili kusaidia kuondoa hali
hiyo kwa Watanzania.
Anatajwa
kama mmoja wa Watanzania wenye mafanikio akiwa miongoni mwa matajiri 10 nchini
hali ambayo binafsi amekuwa akiielezea ni matunda ya juhudi na kujituma, huku
akisema yeye si tajiri bali ni mtumishi katika QG Ltd kama walivyo wengine.
Na bado akapigwa mawe
ReplyDelete