Suleiman Msuya
Paul Makonda |
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda, amesema wako katika mchakato wa kubadili vivutio vilivyoko mkoani humo kuwa vya kitalii ili kuchochea ukuaji uchumi.
Makonda alisema hayo jana wakati akitoa taarifa
kwa vyombo vya habari juu ya ujio wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kesho huku
Rais wa Shelisheli, Danny Faure akija Februari 27.
Makonda alisema Dar es Salaam imekuwa ikipokea
viongozi wengi kutoka ndani na nje ya nchi, hivyo ni wakati mwafaka sasa
kuangalia fursa za kitalii zilizopo.
Alisema Jiji lina vivutio vya asili na
visivyo vya asili na baadhi ya visiwa vikitumika ipasavyo vitachangia uchumi na
maendeleo kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa alitaja baadhi ya maeneo
kama sanamu ya askari, jengo la Karimjee na mengine mengi yakitumiwa vizuri ni
chanzo sahihi cha mapato.
“Tumekuwa tukipokea viongozi kutoka nje
na ndani ya nchi na wananchi lakini ukweli hatujatumia vivutio vilivyopo kuwa
kichocheo cha mapato ya Jiji,” alisema.
Alisema wakati wa kuifanya Dar es Salaam
kama njia umepita hivyo atahakikisha anafanikisha lengo hilo la
kuibadili kuwa Jiji la kitalii.
Makonda alisema pamoja na kulibadilisha
kwa kutumia fursa za kitalii pia anatarajia kuona wananchi wakifaidika moja kwa
moja kwa kuuza bidhaa kwa wageni watakaokuja kulitembelea.
0 comments:
Post a Comment