Fidelis Butahe, Dodoma
KAMATI ya Bunge ya Katiba na Sheria
imebaini matumizi ya fedha za umma yasiyoridhisha kwenye baadhi ya miradi
nchini.
Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa jengo
la Ofisi ya Makamu wa Rais mtaa wa Luthuli, Dar es Salaam, kwa maelezo kuwa
limejengwa chini ya viwango.
Kwa hali hiyo, Kamati imezitaka mamlaka
husika kufanya uchunguzi ili kujiridhisha na matumizi ya fedha za mradi huo na
hatua zichukuliwe kwa watendaji waliohusika na mradi huo.
Akizungumza wakati akiwasilisha taarifa
ya Kamati hiyo bungeni jana, Mwenyekiti wake, Mohamed Mchengerwa alisema Kamati
ilifanya ziara kwenye jengo hilo na kubaini kujengwa chini ya kiwango,
“watendaji wote waliohusika wachukuliwe hatua kali.
“Pia ujenzi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu
wa Serikali. Serikali imekuwa ikiomba fedha Sh bilioni moja kwa ajili ya ujenzi
wa ofisi hiyo kwa miaka mitatu mfululizo.”
Alisema licha ya fedha hizo kuombwa
kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka jana, ofisi hiyo haikupokea kiwango chochote kwa
ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kuhusu miradi ya Dege Eco, Kigamboni,
Mchengerwa alisema ripoti ya uchunguzi wa miradi ya Shirika la Mfuko wa Hifadhi
ya Jamii (NSSF), ukiwamo mradi huo ipo katika hatua za mwisho kukamilishwa na
taasisi zinazofanya uchunguzi.
“Kamati ilitoa muda kwa Serikali
kukamilisha ripoti hizi na inatazamia kupewa taarifa kamili za uchunguzi huu,”
alisema Mwenyekiti wa Kamati.
0 comments:
Post a Comment