Annastazia Maginga, Mwanza
Tundu Lissu |
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama mjini
hapa juzi, Lissu alieleza kuwa uanachama wake TLS unatokana na ada alizolipa na
anaruhusiwa kugombea kwani sheria haijakataza mwanasiasa kugombea.
“Watu wanaoleta hoja za mimi kutogombea kama ni
wanasheria, basi hawajui kutumia uanasheria wao vizuri, kwanza hiki ni Chama
cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na si Tanzania Law Society.
“Ukiwa mwanachama wa chama cha wanasheria, unatakiwa
kulipa kodi na ada na sheria hii haijakataza mimi kugombea eti kwa sababu ni
mwanasiasa,” alisema Lissu.
Alieleza kuwa TLS kimepotea, kwani wao ndio wanaotakiwa
kusimamia na kushughulikia haki lakini huenda anaogopwa kutokana na
misimamo yake ya kikatiba.
“Ni wakati wa kuwa Rais wa TLS, ili kukisimamia chama
hiki kwa kufuata haki kwa mujibu wa sheria na kukabiliana na sheria mbovu zinazotungwa, mtu anayetakiwa
kujua sheria kuliko mtu yeyote yule ni mwanasheria, wao ndio wanatakiwa kujua
sheria zinasemaje,” alisema.
Alihadharisha kuwa endapo chama hicho kitafutwa, inamaana
hakutakuwa na wakili na mambo yote yanayohitaji watu kama hao, hayatafanyika kwa
kuwa mwanasheria katika nchi hii, ni lazima uwe mwanachama wa TLS.
0 comments:
Post a Comment