Peter Akaro
WANAMKE
mmoja aliyejulikana kwa jina la ‘Mama Saidi’ anashikiliwa na polisi kwa tuhuma
za kumuwekea pilipili kwenye macho mtoto wake wa kambo anayesoma darasa la sita
kwa madai ya kutofua nguo za shule.
Tukio
hilo limetokea Mtaa wa Tabata Magharibi na kuripotiwa kwenye ofisi ya Serikali
ya Mtaa huo juzi, kabla ya mwanamke huyo kukamatwa na kupelekwa Kituo cha Polisi
Tabata ambapo anashikiliwa hadi sasa.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum
Amaduni alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema upelelezi bado
unaendelea.
“Mtuhumiwa
atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika, ikiwa ni pamoja na
kupokea taarifa ya daktari ambayo itaonyesha ni kwa kiasi gani mtoto huyo
ameumia au madhara aliyoyapata kutokana na kitendo kile,” alisema Amaduni na
kuongeza:
“Bado
tunakusanya ushahidi, ukikamilika tutapeleka jalada kwa mwanasheria wa Serikali
kwa hatua za mashtaka.”
Awali
majirani walidai imekuwa kawaida kwa mwanamke huyo kumnyanyasa mtoto huyo wa
kambo, lakini Kamanda Amaduni alisema tukio hilo ni la kwanza kuripotiwa kutoka
kwa mwanamke huyo na si kama wanavyoeleza majirani zake.
Mtendaji
wa mtaa huo, Hamza Ramadhani alisema mtoto huyo alipofikishwa ofisini kwake
alikuwa haoni kutokana na athari za pilipili, ndipo alipopelekwa Kituo cha Afya
Tabata.
“Lakini
walipomuangalia waliamua kumpeleka Hospitali ya Amana na taarifa nilizanazo kwa
sasa jana(juzi) amesharuhusiwa yupo nyumbani na mwenzake ila mama ndio bado
yupo polisi,” alisema.
Jirani
wa mtoto huyo, Gowely Anthoy alisema kwa kipindi kirefu kulikuwa na viashiria
vya mtoto huyo kunyanyaswa lakini hakuna aliyeweza kuhoji.
“Mtoto
mwenyewe amekuwa akisema tangu siku nyingi mama hamhudumii ipasavyo, lakini
tulikuwa tukichukulia kama masuala ya kawaida ya watoto, lakini sasa tumejua ni
kweli,” alisema.
0 comments:
Post a Comment