Georgina Misama, Maelezo
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC),
limejipanga kumaliza kero ya makazi ya nyumba kwa Watanzania ifikapo mwaka
2025.
Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba
Tanzania (NHC), Erasto Chilambo, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati
wa mkutano na waandishi wa habari.
Ili kutimiza azma hiyo, Chilambo alisema
nyumba zisizopungua 30,000 zitajengwa kwaajili ya kuuzwa na kupangishwa kwa
watu wa kipato cha chini, kati na juu.
“Katika mkakati huu, Shirika limekusudia
kujenga nyumba 12,000 kwa ajili ya watu wa kipato cha chini; nyumba 13,500 kwa
ajili ya watu wa kipato cha kati na nyumba 2,700, kwa ajili ya watu wenye
kipato cha juu,” alisema Chilambo.
Mbali na nyumba hizo za makazi, Shirika
hilo pia litajenga majengo 1,800 ya kibiashara katika maeneo mbalimbali nchini,
yanayotazamiwa kukamilika ifikapo 2025.
“Katika kuunga mkono uamuzi wa Serikali
wa kuhamia Dodoma, shirika linajenga nyumba za makazi 300, zitakazouzwa kwa
watumishi wa Serikali, ambazo zina ukubwa tofauti zenye vyumba 3 kila moja,”
alisema Charahani.
Tangu kuanzishwa kwa NHC, imekuwa
ikimiliki na kuuza majengo mbalimbali na hivi sasa shirika hilo linamiliki
majengo 2,483 na maeneo 18,121 ya makazi na biashara katika mikoa ya Tanzania
Bara.
0 comments:
Post a Comment