Aidan Mhando, Mwanza
Ansbert Ngurumo |
CHAMA cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Ziwa Victoria kimemuomba Rais John
Magufuli kumkanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ili asije
kuliangamiza Taifa kwa ilichodai kutafuta sifa za kisiasa.
Pia, chama hicho
kimesema Taifa kwa sasa linakumbwa na ugonjwa wa kisiasa hali inayoweza
kuliangamiza kama isipokemewa na anachofanya Makonda kinapaswa kupingwa
vikali na asasi zote ikizingatiwa kwamba Tanzania ni nchi ya kidemokrasia.
Akizungumza kwa
na wanahabari kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kuwa Mwenyekiti wa Chadema
Kanda ya Victoria, Ansebert Ngurumo alisema kinachofanywa na Makonda ni
kutafuta vyeo kwa sifa kwani tangu mwanzo amekuwa akipata vyeo kupitia
'propoganda' za kisiasa bila kutambua yeye ni kiongozi wa kiserikali kwa sasa.
Ngurumo ambaye
aliwahi kuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, alisema Taifa
imekumbwa na ugonjwa wa ukakasi unaowapata viongozi wa kisiasa wanaoitwa
Demagobi.
"Demagogi
ni neno la kigiriki, Demo- watu halafu Gogi- viongozi wanaongoza watu kwa
kutafuta sifa kama akina Makonda. Namuomba Rais Magufuli amkanye asije liingiza
taifa sehemu mbaya kwa kutafuta sifa," alisema.
Akizungumza kwa
kutoa mfano, Ngurumo alisema Joseph McCarthy ambaye alikuwa Senator katika
Bunge la juu Marekani (Senate) 1947 wakati vita baridi ilipopamba moto, alibuni
mbinu ya kupata umaarufu.
Alisema ana
orodha ya Wamarekani wanaoisaliti nchi yao kwa kuwa Wakomunisti na pengine
kufanya upelelezi (espionage) kwa niaba ya Urusi kitu ambacho kipindi kile si
tu kinamaliza wengine kiheshima, lakini pia kinaweza kusababisha hata
kunyang'anywa uraia.
Ngurumo alisema
McCarthy alitaja majina kutoka katika vikaratasi na alipambwa na kupendwa na
sehemu ya umma wa Marekani kwa kuwa kipindi hicho vita dhidi ya USSR ilibeba
hisia kali, ambapo watu hukuweza kuwaambia kitu.
“Huo ndiyo
'ujasiri' aliojifanya anao Senator McCarthy, mpaka kujifaragua kumtaja Waziri
Mkuu wa nchi nyingine, huku baadhi ya wananchi wa US hadi waliandamana kutaka
Senator McCarthy apewe tuzo kwa 'kuongoza mapambano yaliyotukuka dhidi ya
maadui wa US',” alisema.
Katika hatua
nyingine, Ngurumo alivitaka vyombo vya habari kuacha kukuza jambo hilo kwani si
mara ya kwanza taifa kuwa na matukio ya maajabu.
"Mwaka 2013
aliibuka babu wa Loliondo kuwa anatibu magonjwa sugu na taifa zima lilihamia
kwa babu wakiwemo viongozi wakubwa kisiasa, dini na wengineo, huku jambo hilo
likiwa imekuzwa na ‘media’ hivyo nawaomba wanahabari wenzangu fanyeni utafiti
kwanza," alisema.
0 comments:
Post a Comment