Mwandishi Wetu
Profesa Makame Mbarawa |
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ametaka watumishi wa wizara hiyo katika
sekta ya uchukuzi kutumia vizuri fursa ya kuhamia Dodoma kwa kutumikia
Watanzania kwa uadilifu na weledi.
Mbarawa alisema hayo jana Dar es Salaam
wakati akiaga watumishi wa sekta ya uchukuzi wa awamu ya kwanza ambao
wameondoka kwenda Dodoma.
“Nawapongeza kwa kupata fursa ya kuwa
katika awamu ya kwanza katika wizara hii kuhamia Dodoma, fahamuni hii ni fursa
na si changamoto, kwani hatua hii inasogeza huduma karibu na wananchi hivyo
watumikieni kwa moyo,” aliwaasa.
Profesa Mbarawa alisema nia ya Serikali
ni kuhakikisha watumishi wake wanahamia Dodoma na kuendelea na utekelezaji wa
majukumu yake kwa wananchi.
Katibu Mkuu, Dk Leonard Chamuriho alisema
awamu ya kwanza ya watumishi zaidi ya 45 inahamia Dodoma mwezi huu na awamu ya
pili itaanza Machi na watumishi wote wa sekta ya uchukuzi watakuwa Dodoma
Agosti.
“Watumishi wa Sekta ya Uchukuzi
wanaohamia Dodoma katika awamu ya kwanza ni pamoja nami, wakurugenzi na wakurugenzi
wasaidizi, wakuu wa vitengo na maofisa waandamizi,” alisisitiza Dk Chamuriho.
0 comments:
Post a Comment