Edith Msuya
Augustino Mrema |
MWENYEKITI wa Bodi ya Taifa ya Parole,
Augustino Mrema, amesema ni vema sheria ya Parole ikabadilishwa ili wafungwa
wote wanufaike nayo.
Mrema alisema hayo jana Dar es Salaam
wakati akitoa taarifa ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Parole itakayozinduliwa na
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.
Mrema alisema sheria ya kunufaisha
wafungwa ni changamoto kwa Parole ambayo inanufaisha wafungwa wa zaidi ya miaka
minne jambo ambalo si zuri.
“Sheria hii ikifanyiwa marekebisho
itasaidia kwa kiasi kikubwa wafungwa wengine badala ya wa miaka minne pekee,
ili baadaye kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani,” alisema.
Alisema mbali na changamoto hiyo, bado Parole
inakabiliwa na ukosefu wa fedha hali inayosababisha mchakato wa kuwatoa
wafungwa wanaostahili kukwama.
Aliiomba Serikali kuruhusu Bodi hiyo itafute
fedha za kufanya mchakato wa Parole kukamilika ili kuwezesha wafungwa wote
wanaostahili kutolewa magerezani chini ya sheria ya Parole watoke.
“Naomba mfungwa asiendelee kubaki
gerezani wakati anapaswa kutoka chini ya sheria ya Parole na zile Sh milioni
12.8 zilizochangwa na Mchungaji Getrude Lwakatare ni vema zikatumika
kukamilisha mchakato wa Parole kwa wafungwa wa Dodoma na mikoa mingine,” alisema.
Hata hivyo, Mrema aliishauri Polisi kuhusu
suala la dada poa na mashoga kwamba ni vizuri wakakamata wateja wao.
“Kwani ni uonevu kuwakamata peke yao na
kuacha wateja wao ambao ni wanaume kwani dada poa na mashoga ni kikwazo kwenye
mapambano dhidi ya Ukimwi,” alisema.
0 comments:
Post a Comment