Salha Mohamed
MAPAMBANO yaliyoanzishwa ya kudhibiti
dawa za kulevya Mkoa wa Dar es Salaam, yamechukua sura mpya baada ya jana Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutaja watuhumiwa 65 wakiwamo wanasiasa,
viongozi wa dini na kampuni.
Miongoni mwa wanasiasa wanaodaiwa
kujihusisha na utumiaji na uuzaji wa dawa hizo ni Mbunge wa Hai mkoani
Kilimanjaro, mbunge wa zamani wa Kinondoni(CCM), Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo
na Uzima Askofu Josephat Gwajima na Diwani wa Mbagala (CCM), Yusuph Manji
akiwataka kuwataka kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi kesho.
Hata hivyo, katika mkutano wake na
wanahabari jana, Manji alisema atakwenda polisi leo, huku akieleza kuunga mkono
vita dhidi ya dawa za kulevya, lakini akasema utaratibu uliotumiwa na Makonda
umemvunjia heshima.
Kwa upande wake, Gwajima kupitia
msaidizi wake Yekonia Bihagaze alisema wakati ukifika atatoa taarifa rasmi
kuhusu tuhuma hizo.
Naye Mbowe kupitia Katibu Mkuu wa
Chadema, Dk Vincent Mashinji alisema: “Chadema tunalaani kutajwa kwenye tuhuma
za kujihusisha na dawa za kulevya kwamba si la kiungwana ni la kufedhehesha kwa
viongozi.”
Akizungumza jana Makonda alisema Rais
John Magufuli ameonesha dhahiri kutopendezwa na matumizi ya dawa za kulevya
nchini.
Alitaaja wamiliki wa Kampuni za mafuta
na wamiliki kumbi za starehe na hoteli akiwataka kufika polisi kesho.
“Rais alielekeza vyombo vyote na
wananchi kushiriki na kujenga taifa lenye usawa, nguvu kazi na lenye uchumi wa
kati,”alisema.
Alisema wakati wanaanza kupambana na
vita hiyo walianza kupita katika mitaa mbalimbali kuona namna ambavyo tatizo
hilo ni kubwa na kuona namna watu walivyoathirika na dawa hizo.
“Wakati wa ziara ya Dar Mpya kuna mmoja
alikuja kutuonesha namna tumbo lake lilipasuka baada ya vidonge kupasuka
tumboni na kufanyiwa upasuaji,”alisema.
Makonda alisema kampeni hiyo ilianza kwa
kutaja orodha ya wasanii na kuingia mtaani kwa kushuhudia ukubwa wa tatizo hilo
na kupata taarifa sahihi.
Alisema mtu anapoitwa na Mkuu wa Mkoa
anapewa haki yake ya kusikilizwa huku akibainisha kuwa kampeni hiyo si ya
kwenda kimya kimya.
“Watu wanasema hii kitu ningeifanya
kimya kimya lakini hapana kwani tulishafanya kimya kimya tangu mwanzo lakini
tatizo linaendelea kuwa kubwa zaidi,’alisema.
Alilipongeza gazetu hili kwa kuonesha
ushirikiano kwa wenyeviti wa serikali za mitaa kutoa majina katika mitaa yao
ambao wanawasiwasi nao.
Aliwataka wenyeviti hao kutochoka na
kutoa taarifa ndani ya siku kumi na kuanza mchakato wa awamu ya tatu kwa kupita
nyumba hadi nyumba.
Alisema anatamani kuona mtoto wa shule
ya msingi anaelewa kuwa dawa za kulevya ni hatari kwa afya yake pamoja na
kuwabaini.
Alisema wapo vijana waliokiri kutumia
dawa hizo na kuomba kusaidiwa kuacha dawa hizo ikiwemo msanii Khalid Mohamed (TID)
na kukubali kuwasaidia.
“Baadhi yao hadi familia zao ilishaamua
kuwatenga. Ninamaumivu makali sana ninapopita mtaani na kuona mateja wengi
ambao wamezalishwa na watu wenye uchu wa utajiri wa haraka,”alisema.
Alisema
anaimani chini ya Rais Magufuli asiyekuwa na unafiki ataikisha nchi salama na
dawa za kulevya kuwa historia katika serikali yake.
Makonda alifafanua kuwa zipo njia
mbalimbalia ambazo amegundua hutumika kuigiza au kusafirisha dawa za kulenya
kupitia Dar es Salaam.
“Nimekuwa operesheni usiku na mchana
hatulali saa zote ili kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa salama. Imegundulika
ipo sehemu ya kuingiza dawa kirahisi ambayo ni Dar es Salaam,”alisema.
Alisema watu hununua dawa kutoka
Pakistani na kuja na meli ambayo inakuwa na mzigo na kuchukua boti zao kuingiza
kwenye boti na kupakia kwenye mapipa ambapo meli inapokaribia bandarini
huyatupa Zanzibar, Bagamoyo na Tanga yakiwa na GPRS.
“Wakija kwenye bandari zetu wanakuwa
hawana dawa wakifika wanapakuwa mizigo yao kama kawaida halafu waliokubaliana
huenda kwenye yale mapipa wakiwa na GPRS iliyofungwa nay ale mapipa na kuyaokoa
na kuyachukua,”alisema.
Alisema baada ya kuyachukua huyaweka
sawa na kuyasafirisha Afrika Kusini kupitia Mtwara.
“Njia ya pili hutumia magari kwa kununua
Japan na kuzunguka nayo, wengine husafirisha kupitia meli za mafuta, wengine
huwa na boti zao,’alisema.
Alisema wengine hutumia wasichana kwa
kuwasafirisha nchini China akidai anachukua biashara nchini China.
Makonda alisema hakuna jiwe
litakalosalia juu ya jiwe katika kampeni ya kutokomeza dawa za kulevya, kwa mtu
mwenye jina kubwa au dogo endapo taarifa zao zitakuwa na mashaka au kupata
uchunguzi zaidi na kuwaachia wasiokuwa na hatia.
Alisema wapo waliokuwa nje ya nchi ambao
walitakiwa kuripoti kituo cha polisi pindi watakapotua uwanja wa ndege
wakamatwe.
“Wale waliokuwa wamejificha mahala
tutawatafuta na tutawapata.Vita hii tukishindwa hajashindwa Makonda kwani wapo
wanaodai kuwa hawezi,”alisema.
0 comments:
Post a Comment