Sharifa Marira
Dk Hamis Kigwangalla |
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam linawasaka wanaume wanaodaiwa kufanya mapenzi kinyume cha maumbile au
‘mashoga’ na kujitangaza kwenye mitandao ya kijamii.
Hao ni wale ambao walitakiwa kuripoti
kituoni hapo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dk Hamis Kigwangalla, lakini hawakutii.
Washukiwa hao waliotajwa majina yao juzi
na Kigwangalla ni James Charles ‘James
Delicious’, Godfrey Majunga ‘Kaoge’ na Daniel Claud ‘Dani Mtoto wa Mama’.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar
es Salaam, Kamanda wa Kanda hiyo, Simon Sirro alisema ni kosa kufanya mapenzi
kinyume cha maumbile, hivyo vijana wake wameshaingia mtaani kuwatafuta watu
hao.
‘’Sambamba na agizo la Naibu Waziri,
tulishaanza kushughulikia suala hilo na sasa askari wetu wako maeneo mbalimbali
kusaka mashoga, hivyo tutawakamata wote wanaofanya hivyo, wakiwamo waliotajwa
ambao wamekuwa wakijitangaza kwenye mitandao ya kijamii,’’ alisema Kamanda Sirro.
‘’Suala hili tunalishughulikia kwa
ukaribu, naombeni hata ninyi kama mnafanya mwache tutawashughulikia bila
kujali, timu yetu ya mambo ya makosa ya kimtandao imeshawatambua wote
wanaofanya hivyo mitandaoni hata kama hawajatajwa,’’ aliongeza
Alieleza kuwa ni lazima kuheshimu sheria
na kuacha kuiga mambo ya kigeni ambayo hayana faida na yenye madhara makubwa
kiafya.
0 comments:
Post a Comment