RIPOTI ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya Desemba
mwaka jana imebaini kuporomoka kwa idadi ya wateja wa kampuni za simu nchini.
Hata hivyo imebainisha kuwa kampuni ya Vodacom Tanzania pekee
ndiyo imezidi kupata wateja wengi.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, idadi ya watumiaji wa huduma
za simu za mkononi imepungua kutoka 40,560,368 Novemba mwaka jana hadi 40,173,783
Desemba wakipungua wateja 387,000.
Ilibainishwa kuwa pamoja na upungufu huo wa wateja, Vodacom
imeendelea kupata wapya ikisajili 64,951 na kuongezeka kutoka 12,354,474 hadi
12,419,425.
Tigo ina wateja 11,677,344 huku Airtel ikiwa na asilimia 26 ya
soko la watumiaji simu na kampuni mpya ya Halotel ikifikisha idadi ya wateja
11,020 katika kipindi hicho.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika robo ya mwisho ya mwaka
jana matumizi ya simu yaliporiomoka ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka juzi.
Kwa upande wa matumzi ya huduma za kifedha kupitia simu
za mkononi, ripoti ya TCRA ilibainisha kuwa hadi mwishoni mwa mwaka jana, huduma
ya M-Pesa ya Vodacom iliongoza katika soko kwa asilimia 45, Tigopesa asilimia
52.6 na Airtel Money asilimia 40.3.
Akizungumza kuhusu ripoti hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano
na Uhusiano wa Vodacom, Rosalynn Mworia alisema
ni fahari kwao kuona bado wanakubalika kwa Watanzania wengi na kuendelea kuwa
kinara wa kampuni za mawasiliano nchini katika robo ya mwisho ya mwaka jana
licha ya changamoto zilizopo kenye masoko.
“Mafanikio haya yanadhihirisha kuwa tunaongoza kwa kubuni
na kutoa huduma bora zinazokwenda sambamba na mahitaji ya soko la mawasiliano,
na dhamira yetu ya kuipeleka Tanzania
katika ulimwengu wa kidigitali kupitia ubunifu wa teknolojia ya mawasiliano, ili kukidhi haja
za wateja wetu,” alisema Mworia.
0 comments:
Post a Comment