Washington, Marekani
Rais Donald Trump |
MAHAKAMA ya rufani nchini Marekani imetupilia
mbali rufaa ya Rais Donald Trump kutaka kuendelea kutekelezwa kwa amri yake ya
kuzuia wakimbizi, hasa kutoka kwenye mataifa ya Kiislamu kuingia nchini humo.
Kwa siku mbili mfululizo, miji miwili ya
Washington na Minnesota ililaumu hatua hiyo ya Trump na wakaamua kwenda
kufungua kesi kwenye moja ya mahakama mjini Seattle dhidi ya amri yake hiyo ya
kuwazuia Waislamu.
Hata hivyo, Trump akishirikiana na timu
yake ya haki na sheria waliamua kukata rufaa ya kupinga zuio hilo la mahakama
wakishinikiza kuwa amri hiyo ya rais, iendelee kufanya kazi.
Mahakama imeeleza kuwa rufaa ya Trump
ilikosa mashiko ya kikatiba na hivyo ikatoa siku moja hadi leo kuwasilishwa
utetezi zaidi kuhusu nini wanakitaka katika rufaa yao.
Watu wenye pasi halali za kusafiria
kutoka katika mataifa saba yaliyopigwa marufuku kuingia Marekani waliendelea
kusota na kupata usumbufu licha ya mahakama kuweka zuio la kusitisha amri hiyo.
Amri ya Trump ambayo aliitoa mapema wiki
iliyopita ilisababisha vurugu na maandamano makubwa kutoka kwenye maeneo
tofauti duniani, ikiwemo Marekani katika miji kadhaa na viwanja vya ndege.
Juzi kulikuwa na maandamano makubwa
katika miji ya Washington na Miami nchini Marekani na kwenye miji mingine
kadhaa barani Ulaya.
Barani Ulaya maandamano hayo yameripotiwa
kufanyika katika miji ya London, Paris, Stockholm na Barcelona. Hata hivyo,
wakati watu hao wakiandaman kumpinga, wafuasi wa rais huyo mpya nao waliingie
mitaani maeneo mbalimbali kumuunga mkono.
Tangu Trump asaini amri yake hiyo ya
kuwazuia wakimbizi kuingia Marekani, tayari viza 60,000 zimefutwa au kuzuiwa
kutolewa.
Hata hivyo, mara baada ya hakimu James
Robert kutoa mwito wa kuomba vyombo vya sheria kuweka zuio la muda la kusitisha
amri hiyo ya rais, mwito huo ulifanikiwa na amri hiyo kuwekwa pembeni kwa muda.
Trump alichukizwa na hatua ya Robert na
kumtaka arudishe amri yake iendelee kufanya kazi.
Zuio la siku 90 aliloweka Trump liliwalenga
wakimbizi na raia wa mataifa saba ya Kiislamu ambayo ni Iraq, Iran, Syria,
Yemen, Somalia, Sudan na Libya.
Mashirika makubwa ya usafiri wa ndege
bado yanawakubalia raia kutoka mataifa hayo husika, kusubiri ndege na kuingia
Marekani.
Rufaa ilyokatwa na Serikali kupinga amri
ya mahakama iliwasilishwa rasmi na kitengo cha haki na sheria cha Marekani.
Trump ametajwa kuwa ni mmoja kati ya
waliokata rufaa hiyo sambamba na wengine kama vile Waziri wa Nyumba na Makazi,
John Kelly pamoja Rex Tillerson.
Maelezo ya rufaa hiyo yanasema kuwa amri
ya rais kukataza wakimbizi wasiingie Marekani ni kwa nia njema tu ya kutaka
nchi kuwa salama.
Mbali na hivyo, Trump pia alionekana
kuanzisha vita ya maneno dhidi ya hakimu, Robert kupitia mtandao wa twitter.
“Haya maoni ya kutoka kwa majaji
yanayodai kutetea haki za binadamu ni ya kipuuzi dhidi yetu na kwa uwezo wetu
tutayashinda,” alisema.
Trump aliongeza kuwa hawezi akafanya
kazi na mahakimu ambao hawana uchungu na ulinzi wa taifa lao kwa kuruhusu kila
mtu kuingia akieleza kuwa kufanya kufanya hivyo kutotoa fursa kwa wabaya na
wema kuingia Marekani.
Alimalizia kwa kusema kuwa ana imani
rufaa yao itashinda kitu ambacho kimekuja kuwa kinyume na matarajio.
0 comments:
Post a Comment