Christina Mseja
Lipumba na Maalim Seif |
KATIBU Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, amesisitiza
kuwa haoni sababu ya kukutana na Profesa Ibrahim
Lipumba kuzungumzia mambo ya chama kwa kuwa si mwanachama halali wa CUF hivi
sasa.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam
jana, ilisema Maalim Seif alitoa kauli hiyo kwenye ziara ya siku nne kwenye
wilaya saba za mikoa mitatu ya Unguja.
Maalim alisema ataendelea kufuata taratibu za kisheria ili kuhakikisha chama kinamaliza
moja kwa moja mgogoro aliodai umepandikizwa na CCM kupitia kwa Lipumba.
Alitaka
wapenzi na wanachama wa CUF kuunga mkono jitihada zinazofanywa na chama kupigania demokrasia ya
kweli nchini.
Aliwataka wanachama wa CUF kushirikiana na viongozi wakuu wa CUF wanaotambuliwa na Baraza
Kuu la Uongozi kujenga na kuimarisha chama hicho.
Alifafanua
kuwa wakati anaendelea kuimarisha chama kupitia viongozi halali, ni vema wasiwe
na wasiwasi na uamuzi walioufanya kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka juzi
kwa kuipa CUF ushindi wa urais wa Zanzibar kuwa hautapuuzwa.
Aliwataka
kuendelea kuwa watulivu na kuwahakikishia kuwa siku chache zijazo haki yao
itapatikana. "Nawahakikishia, tumepigana vya kutosha katika kudai haki yetu
na tumefikia hatua nzuri za kupata haki yenu.
“Hatua
ya wananchi wa Zanzibar ya kuipa ushindi CUF ni kutokana na CCM kushindwa kuongoza
Wazanzibari kwa misingi ya haki, usawa na demokrasia,” alisema.
Alifafanua kuwa mgogoro wa
uongozi ndani CUF uliotokana na hatua ya Profesa Lipumba kuamua kurudi
katika nafasi ya uenyekiti wa chama hicho na kusema watahakikisha wanapata
ushindi.
“Lipumba alijiuzulu mwenyewe
hivyo hakuna hoja yoyote ya kisheria inayomwezesha kurudi tena katika nafasi
hiyo,” alisema.
Maalim Seif ataendelea na ziara hiyo katika Wilaya ya
Magharibi ‘A’, ‘B’ kisiwa cha Unguja, Pemba hadi Februari 24.
Pamoja na kufanya ziara hiyo na kuzungumza na viongozi wa
chama na jumuiya zake, Katibu atafanya uzinduzi na uimarishaji wa waratibu wa chama.
0 comments:
Post a Comment