Salha Mohamed
TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI),
imepokea msaada wa Sh. milioni 303 kwa ajili ya upasuaji wa watoto 138 wenye
matatizo ya moyo nchini.
Fedha hizo zilizotolewa na taasisi za I
& M Bank, Baps Charities na Youth walfare Trust, zitasaidia kupunguza
gharama za upasuaji kwa watoto hao iwapo wagepata huduma hiyo nje ya nchi.
Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Profesa Mohamed
Janabi alisema kabla ya Novemba watakuwa wamefanya upasuaji kwa watoto hao ili
kuokoa maisha yao huku akizitaka taasisi zingine kujitokeza kusaidia.
“Awamu ya kwanza ilikuwa na wagonjwa
watoto 500 huku wengine 211 wakiwa ni
watu wazima. Tayari tumehudumia wagonjwa wa moyo 728 katika kipindi cha miezi
tisa cha Januari hadi Septemba mwaka huu,” alisema Profesa Janabi.
Alisema wagonjwa hao kama wangepatiwa
huduma hiyo nje ya nchi, wangetumia sh. milioni 23 kila mmoja na kwamba huenda
wengine wangefariki kutokana na kushindwa kwenda kutibiwa.
“Tumefanya upasuaji lakini fedha tunazopata
hazikamilishi gharama zote, bali imesaidia kwa kiasi kikubwa kununua vifaa vya
upasuaji,”alisema.
Mkurugenzi wa Utafiti JKCI, Dk Pedro
Pallangyo alisema mwaka jana walitoa huduma ya Cath Lab(upasuaji bila kupasua
kifua) kwa wagonjwa 234 ambapo kwa mwaka huu Januari hadi Septemba walitoa
huduma kwa wagonjwa 494.
“Hii ni zaidi ya mara nne ya tuliyofanya
mwaka jana, kwa huduma ya kupasua kifua
mwaka jana tulihudumia wagonjwa 204 mwaka huu miezi 9 ya kwanza tumehudumia
wagonjwa 234 sawa na ongezeko la asilimia 116 ukilinganisha na mwaka
jana,”alisema.
Alishukuru Taasisi ya I&M Bank kwa
kutoa Sh milioni 33 zitakazo saidia kufanya upasuaji kwa watoto 15, Taasisi ya
Youth Walfare Trust iliyotoa Sh milioni 48.4 zitakazosaidia upasuaji kwa watoto
22.
Pia aliipongeza taasisi ya Baps Charity
kwa kutoa Sh milioni 222 kwa ajili ya upasuaji wa watoto 101, huku taasisi hiyo
ikifanya muendelezo wa kile ambacho walifanya awali kwa kutoa kiasi kama hicho
na kufanyiwa upasuaji watoto 100.
Alisema kama idadi ya wagonjwa
waliopimwa magonjwa ya moyo na kuhitaji kufayiwa upasuaji hawataongezeka
zitahitajika zaidi ya Sh milioni 800 kufaya upasuaji wa moyo na kubainisha kuwa
uhitaji utakuwepo kwani magonjwa hayo hayajaisha.
Mama mzazi wa Mtoto John Mayatab mwenye
umri wa miezi nane, anayesumbuliwa na matatizo zaidi ya manne kwenye moyo,
Neema Daudi alisema tatizo la mtoto wake liligundulika akiwa na mwezi mmoja,
ambapo alikuwa anashindwa kunyonya huku akitokwa na jasho hata kama hakuna
joto, hivyo aliitaka jamii kupima afya za watoto wao.
0 comments:
Post a Comment