Joyce Kasiki, Dodoma
MFUKO wa
Pensheni wa LAPF umefanya uwekezaji wa miradi yenye thamani ya zaidi ya
shilingi bilioni 60 katika sekta ya elimu mkoani Dodoma.
Uwekezaji huo
umehusisha ujenzi wa nyumba 15, majengo mawili ya hosteli, viwanja vya michezo,
sehemu ya kuogelea na barabara zenye urefu wa kilomita 5.4 katika Chuo cha
Serikali za Mitaa Hombolo.
Aidha, LAPF
katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), imejenga majengo mawili ya hosteli kwenye
Chuo cha Afya, madarasa na maabara ya kufanyia mafunzo ya miili kwa vitendo.
Mfuko huo ambao
kwa asilimia 86 umewekeza katika maeneo mbalimbali nchini, pia una mikakati
mbalimbali, ikiwemo kuwekeza katika viwanda ili kutimiza azma ya Serikali ya
kufikia Tanzania ya Viwanda.
Kaimu Mkurugenzi
wa huduma za wanachama wa mfuko huo, Ramadhan Mkeyenge alisema alipokuwa
akitembelea miradi hiyo kuwa katika mkakati huo tayari mfuko umeshafanya utafiti
wa awali wa kujenga kiwanda cha chai wilayani Lushoto na kamba mkoani Tanga. Gharama
za uwekezaji huo ni shilingi bilioni 7.4.
Mkeyenge
alisem kuwa mfuko huo unakuwa kwa kasi na kubainisha kuwa kuanzia 2008
mpaka Oktoba 2016, umekua kwa asilimia 80; kutoka shilingi bilioni 216 mpaka
kufikia trilioni 1.12 na kuufanya uwe na uwezo wa kulipa pensheni za wastaafu kwa
miaka 100 ijayo bila kutetereka.
“Shughuli zetu
zote tunazozifanya, zinategemea michango kutika kwa wananchama, vitega uchumi
vilivyokomaa , mikopo na uwekezaji uliofanyika katika maeneo mbalimbali,
"Na kiwango
kikubwa cha asilimia 44 tumewekeza kwenye amana za Serikali kutokana na kuwa ni
sehemu salama zaidi na yenye kurudisha hela kwa wakati." alisema
Kifungumali
“Wanawakeza
kwenye miradi mbalimbali kwa njia ya ubia upo mradi wa standi ya Msamvu Mkoani
Morgoro amba ilianza mwaka 2012 na umegharimu kiasi cha shlingi bilioni 12
awamu ya kwanza, Mwanza complex-bilioni 64 na umekabidhiwa septemba mwaka huu.
Kifungumali
alisema,mipango ya baadaye ya mfuko huo ni kujenga jengo la ofisi mkaoni Arusha
,kuwa na madi wa kisasa Buguruni na kuwekeza kwenye amana mbalimbali kwenye
Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana
nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment