Leonce Zimbandu
Valentino Mlowola |
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais
Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki ameagiza
Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza watendaji Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf).
Akipokea ripoti ya utekelezaji wa Mpango
wa Tatu wa Kunusuru Kaya Maskini katika Mtaa wa Mambo Leo B Kata ya Sandali,
Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam jana, Kairuki alisema baadhi ya
watendaji hao wanatuhumiwa kwa kujinufaisha kwa rushwa wakati wa utekelezaji.
Mpango huo ulianza kuendeshwa kuanzia
Julai 2015 hadi sasa lakini imebainika zipo kaya zimeingizwa kinyemela baada ya
wahusika katika kaya hizo kutoa kamisheni kwa watendaji wa Tasaf.
Alisema mtaa huo ulikuwa na wanufaika 118
lakini kuna kaya 40 zilibainika kuingizwa bila kukidhi vigezo, hivyo zinapaswa
kurejesha fedha hizo ili wanufaika wengine wapewe.
“Nahitaji Jeshi la Polisi na Takukuru wachukue
hatua za haraka kuchunguza na iwapo itabainika rushwa hatua zichukuliwe mara
moja,” alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaviva allisema
watatekeleza agizo hilo la waziri kwa kuhakikisha vyombo vya dola katika
Manispaa hiyo vinachukua hatua ya kuwakamata ili kuwahoji watuhumiwa.
“Kuanzia sasa naikabidhi kazi hiyo kwa
Ocd wa Temeke na Afisa Takukuru Wilaya ya Temeke kushughulikia shuala hilo
haraka kwa kuchukua majina ya wanufaika wa mpango huo,” alisema.
Awali Diwani wa kata hiyo, Wilbert
Tarimo alisema kuwa wakazi wa kata hiyo wanakabiliwa na changamoto mbili,
ikiwamo nyumba zao kuwekewa alama X na Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia
(Tazara) bila taarifa.
Changamoto nyingine kukosa eneo la
kujenga Kituo cha Afya na kisima cha maji kushindwa kukamili na kusababisha
usumbufu wa maji katika eneo hilo.
Alisema kitendo cha kuwekewa X
kinawafanya wakazi wa eneo hilo kuishi kwa wasiwasi kwa kuhofia kubomolewa,
hivyo wanaiomba serikali kuwasaidia.
“Tunakuomba Waziri utusaidie kwa kuwa
kila tunapofuatilia hatupati majibu, hivyo wananchi hao wanahitaji majibu,”
alisema.
Akikijibu malalamiko hayo, Waziri
Kairuki alisema ataandika barua mbili; moja kwa Waziri wa Uchukuzi, Profesa
Makame Mbarawa na nyingine kwa waziri Kilimo, Mifugo na Uvuzi Dk. Charles
Tizeba ili kushughulia changamoto hizo.
0 comments:
Post a Comment