Abraham Ntambara
William Mwamalanga |
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetakiwa kuacha vita ya
maneno na vyama vya upinzani, badala yake wamsaidie Rais katika kutatua
changamoto zinazowakabili wananchi.
Hayo yalielezwa
na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste Tanzania,
William Mwamalanga alipozungumza
jana na JAMBO LEO.
Askofu Mwamalanga alisema CCM wanapaswa kuchapa kazi na
siyo kuchonga maneno na wapinzani.
“CCM wanapenda malumbano na vyama vya upinzani kiasi cha kila
kukicha wanatafuta sababu kwa kufanya malumbano hayo,” alisema Mwamalanga.
Mwamalanga alisema kwamba CCM, wanashindwa kumsaidia Rais
mambo mengi na hawajui kama kuendeleza malumbano hayo ni dalili ya kushindwa
kuisaidia serikali yao katika kutekeleza majukumu.
Alifafanua kuwa chama tawala ndiyo msaidizi wa Rais kwa
mambo ya ushauri, kutatua kero za wanyonge na misaada kwa wananchi wahitaji
badala yake kimekuwa hakifanyi hivyo na nidhahiri hakipo karibu na wananchi
wanyonge.
Alisema CCM wanatakiwa si kila suala linalozungumzwa na
wapinzani na wao waibuke na kuwajibu inatakiwa watambue kuwa uchaguzi ulikwisha
hivyo watekeleze ahadi zao za kwenye Irani yao ya uchaguzi huku wakiwasubiri
wapinzani kupambana nao katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020.
Alisesitiza kwamba chama tawala kinatakiwa kupambana katika
kuwajibika kwenye kazi ili wawadehihirishie wananchi na wapinzani kwa
uchapakazi wao kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
Askofu Mwamalanga alibainisha maisha ya watu kwa hivi
sasa nchini wanahali mbaya kutokana na ugumu wa kiuchumi unaowakabili hivyo
ingetegemewa kuona ni namna gani serikli inatoa majibu juu ya hali hii kwa
wananchi.
Aidha aliwataka watambue kuwa viongozi wa vyama vya
upinzani wanafanya wanapowasema wanakuwa na lengo la kuwachokoza ili washindwe
kufanya kazi na hivyo kuingia katika mtego wao na kulumbana wakati wananchi
siyo hitaji lao.
Alisema hivi sasa watu wanaona Rais yuko peke yake na
hakuna wanaomsaidia ambao aliongeza hadi leo watu wanalalamika kwa nini rais
hajafika Kagera ambapo alifafanua kuwa hayo ndiyo yanegekuwa masuala ya
kuzungumza kwenye chama.
Mwamalanga alisema ingetegemewa Katibu Mkuu, Msemaji na
viongozi wengeine wa chama wangekuwa huko Kagera kama chama tawala kikiongoza
katika misaada ku badala yake hawajafanya chochote wamemuachia Mkuu wa mkoa tu.
Alisema Kama viongozi wa dini wameona suala hilo siyo
sahihi ambapo wamewataka CCM kama chama tawala kuwa mstari wa mbele katika utekelezaji
wa maagizo ya Rais.
0 comments:
Post a Comment